Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 20:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, wanaume elfu ishirini na sita waliokuwa na silaha, mbali na hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Watu wa kabila la Benyamini walikusanya kutoka miji yao jeshi la watu 26,000 wenye kutumia silaha, nao wakazi wa mji wa Gibea wakakusanya watu 700 waliochaguliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Watu wa kabila la Benyamini walikusanya kutoka miji yao jeshi la watu 26,000 wenye kutumia silaha, nao wakazi wa mji wa Gibea wakakusanya watu 700 waliochaguliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Watu wa kabila la Benyamini walikusanya kutoka miji yao jeshi la watu 26,000 wenye kutumia silaha, nao wakazi wa mji wa Gibea wakakusanya watu 700 waliochaguliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu elfu ishirini na sita kutoka miji yao waliojifunga panga, mbali na hao vijana wenye uwezo mia saba kutoka wale walioishi Gibea.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Siku ile Wabenyamini wakakusanya watu 26,000 kutoka miji yao, waliojifunga panga, mbali na hao 700 waliochaguliwa miongoni mwa hao waliokaa Gibea.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 20:15
9 Marejeleo ya Msalaba  

Katika wana wa Benyamini, vizazi vyao, kwa kufuata jamaa zao, na nyumba za baba zao, kama hesabu ya majina, kuanzia umri wa miaka ishirini na zaidi, wote walioweza kwenda vitani;


wale waliohesabiwa katika kabila la Benyamini, walikuwa watu elfu thelathini na tano na mia nne (35,400).


na jeshi lake, na wale waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu thelathini na tano na mia nne.


Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia sita.


Lakini wana wa Benyamini wakakutanika huko Gibea kutoka katika miji yao, ili watoke kwenda kupigana na wana wa Israeli.


Lakini watu hao, watu wa Israeli, walijitia nguvu, wakaviandaa vile vita mara ya pili mahali pale walipojiandaa siku ya kwanza.


Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea siku ya pili, wakawaua watu elfu kumi na nane tena katika watu wa Israeli; hao wote walikuwa wamejihami.


BWANA akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza wanaume elfu ishirini na tano na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo