Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 2:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Watu hao wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioendelea siku zao baada ya Yoshua, hao waliokuwa wameiona hiyo kazi kubwa ya BWANA yote, aliyokuwa ameitenda kwa ajili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu siku zote za maisha ya Yoshua na baada ya kifo chake muda wote walioishi wale wazee waliosalia ambao waliyaona matendo makuu ambayo Mwenyezi-Mungu aliwatendea Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu siku zote za maisha ya Yoshua na baada ya kifo chake muda wote walioishi wale wazee waliosalia ambao waliyaona matendo makuu ambayo Mwenyezi-Mungu aliwatendea Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Waisraeli walimtumikia Mwenyezi-Mungu siku zote za maisha ya Yoshua na baada ya kifo chake muda wote walioishi wale wazee waliosalia ambao waliyaona matendo makuu ambayo Mwenyezi-Mungu aliwatendea Waisraeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Watu wakamtumikia Mwenyezi Mungu siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, wale waliokuwa wameona mambo makuu ambayo Mwenyezi Mungu alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Watu wakamtumikia bwana siku zote za maisha ya Yoshua, na za hao wazee walioishi baada ya Yoshua kufa, waliokuwa wameona mambo makuu ambayo bwana alikuwa ametenda kwa ajili ya Israeli.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 2:7
8 Marejeleo ya Msalaba  

Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zake zote Yehoyada kuhani alizomfundisha.

Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa BWANA siku zote za Yehoyada kuhani.

Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.

Nao Israeli wakamtumikia BWANA siku zote za Yoshua, na siku zote za hao wazee walioishi baada ya kufa kwake Yoshua, hao walioijua kazi yote ya BWANA, aliyowatendea Israeli.

Lakini hawakuwasikiliza hao waamuzi wao, maana walifanya uasherati kwa kuifuata miungu mingine, wakajiinamisha mbele yao; wakageuka upesi, na kuiacha njia ile waliyoiendea baba zao, waliozitii amri za BWANA bali wao hawakufanya hivyo.

Basi hapo Yoshua alipowapa watu ruhusa waende zao, wana wa Israeli wakaenda kila mtu kuuendea urithi wake, ili kuimiliki hiyo nchi.

Kisha Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa BWANA, akafa, naye alikuwa na umri wa miaka mia moja na kumi.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo