Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 2:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 mimi nami tokea sasa sitalifukuza taifa mojawapo la hayo aliyoyaacha Yoshua alipokufa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 sitayafukuza tena mataifa ambayo Yoshua aliyabakiza, wakati alipofariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 sitayafukuza tena mataifa ambayo Yoshua aliyabakiza, wakati alipofariki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 sitayafukuza tena mataifa ambayo Yoshua aliyabakiza, wakati alipofariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 mimi nami sitafukuza taifa lolote ambalo Yoshua aliliacha alipofariki.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 2:21
8 Marejeleo ya Msalaba  

kwa sababu hawakuzitekeleza hukumu zangu, bali walizikataa amri zangu, nao walizitia unajisi sabato zangu, na macho yao yaliandama vinyago vya baba zao.


jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi.


Tazama, nimewagawieni kwa kura mataifa haya yaliyobaki, yawe urithi kwa makabila yenu, toka mto wa Yordani, pamoja na mataifa yote niliyowakatilia mbali, mpaka bahari kubwa upande wa magharibi.


Yeye BWANA, Mungu wenu, atawatoa kwa nguvu mbele yenu, atawafukuza wasiwe mbele ya macho yenu tena; nanyi mtaimiliki nchi yao, kama BWANA Mungu wenu, alivyowaambia.


Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza BWANA, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao?


Basi kwa ajili ya hayo mimi nilisema zaidi, Mimi sitawafukuza watoke mbele zenu; lakini watakuwa kama miiba mbavuni mwenu, na miungu yao itakuwa ni mtego kwenu.


Basi haya ndiyo mataifa ambao BWANA aliwaacha, ili awajaribu Israeli kwa hao, yaani, awajaribu hao wote ambao hawakuvijua vita vyote vya Kanaani;


aliwaacha wakuu watano wa Wafilisti, na Wakanaani wote, na Wasidoni, na Wahivi waliokaa katika kilima cha Lebanoni, toka mlima wa Baal-hermoni mpaka kuingia Hamathi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo