Waamuzi 19:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC9 Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria wake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu. Tazama suraMatoleo zaidiBiblia Habari Njema9 Huyo Mlawi na suria wake pamoja na mtumishi wake walipoinuka kwenda zao, baba mkwe wake akamwambia huyo Mlawi, “Sasa mchana umekwisha na jioni imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubuhi utaamka mapema kuanza safari yako ya kurudi nyumbani.” Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND9 Huyo Mlawi na suria wake pamoja na mtumishi wake walipoinuka kwenda zao, baba mkwe wake akamwambia huyo Mlawi, “Sasa mchana umekwisha na jioni imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubuhi utaamka mapema kuanza safari yako ya kurudi nyumbani.” Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza9 Huyo Mlawi na suria wake pamoja na mtumishi wake walipoinuka kwenda zao, baba mkwe wake akamwambia huyo Mlawi, “Sasa mchana umekwisha na jioni imekaribia. Ulale hapa, na kufurahi. Kesho asubuhi utaamka mapema kuanza safari yako ya kurudi nyumbani.” Tazama suraNeno: Bibilia Takatifu9 Kisha yule mtu alipoinuka aende zake pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani baba wa yule msichana, akamwambia, “Tazama sasa jioni inakaribia. Ulale hapa, usiku unakaribia. Ukae, ukajifurahishe nafsi yako. Kesho unaweza kuamka asubuhi na mapema uende nyumbani kwako.” Tazama suraNeno: Maandiko Matakatifu9 Basi wakati yule mtu alipoinuka aende zake, pamoja na suria wake na mtumishi wake, baba mkwe wake, yaani, baba wa yule msichana akamwambia, “Tazama sasa jioni inakaribia. Ulale hapa usiku unakaribia. Ukae, ukajifurahishe nafsi yako. Kesho unaweza kuamka mapema asubuhi na uende nyumbani kwako.” Tazama sura |