Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 19:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Naye alipotazama, akamwona huyo mtu msafiri katika eneo la mji lililokuwa wazi; huyo mzee akamwuliza, Unaenda wapi na umetoka wapi?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Mzee huyo alipotazama na kumwona huyo msafiri akiwa huko uwanjani, alimwuliza, “Umetoka wapi na unakwenda wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Mzee huyo alipotazama na kumwona huyo msafiri akiwa huko uwanjani, alimwuliza, “Umetoka wapi na unakwenda wapi?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Mzee huyo alipotazama na kumwona huyo msafiri akiwa huko uwanjani, alimwuliza, “Umetoka wapi na unakwenda wapi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Alipotazama na kuwaona hao wasafiri katika uwanja wa mji, yule mzee akawauliza, “Ninyi mnaenda wapi? Nanyi mmetoka wapi?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Alipotazama na kuwaona hao wasafiri katika uwanja wa mji, yule mzee akawauliza, “Ninyi mnakwenda wapi? Nanyi mmetoka wapi?”

Tazama sura Nakili




Waamuzi 19:17
7 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia, Hajiri, wewe mjakazi wa Sarai, unatoka wapi, na unakwenda wapi? Akanena, Namkimbia bimkubwa wangu Sarai.


Akamwagiza yule wa kwanza akasema, Esau, ndugu yangu, akikukuta, na kukuuliza, akisema, Wewe ni wa nani? Unakwenda wapi? Tena ni wa nani hawa walio mbele yako?


Kisha msafiri mmoja akamfikia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikia.


Njia kuu zimeachwa, msafiri ameikimbia barabara; ameyavunja maagano, ameidharau miji, hamjali mtu.


Wewe uliye tumaini la Israeli, wewe uliye Mwokozi wake wakati wa taabu, kwa nini wewe umekuwa kama mtu akaaye katika nchi, kama mgeni, na kama mtu mwenye kusafiri, ageukaye upande ili kukaa usiku mmoja tu?


Kisha, tazama, akatokea mwanamume mzee, akitoka kazini kwake shambani, wakati wa jioni; mtu huyo alikuwa ni wa ile nchi ya vilima vilima ya Efraimu, naye alikuwa anakaa katika Gibea kama mgeni lakini wenyeji wa mahali hapo walikuwa Wabenyamini.


Akamwambia, Sisi tunapita hapa kutoka Bethlehemu-yuda, tunaenda huko upande wa mbali wa nchi ya vilima vilima ya Efraimu; ndiko nilikotoka nami nilikwenda Bethlehemu-yuda; nami sasa naiendea nyumba ya BWANA, wala hakuna mtu anikaribishaye nyumbani mwake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo