Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 19:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Bwana wake akamwambia, Hatutageuka sisi kuingia mji wa wageni, ambao si wa wana wa Israeli; lakini tutapita mpaka Gibea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Bwana wake akamjibu, “Hatutageuka na kuingia katika mji wa wageni ambao si Waisraeli. Tutaendelea na safari mpaka Gibea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Bwana wake akamjibu, “Hatutageuka na kuingia katika mji wa wageni ambao si Waisraeli. Tutaendelea na safari mpaka Gibea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Bwana wake akamjibu, “Hatutageuka na kuingia katika mji wa wageni ambao si Waisraeli. Tutaendelea na safari mpaka Gibea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Lakini bwana wake akamjibu, “Hapana. Hatutaingia kwenye mji wa kigeni, ambao watu wake si Waisraeli. Tutaendelea hadi Gibea.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Lakini bwana wake akamjibu, “Hapana. Hatutaingia kwenye mji wa kigeni, ambao watu wake si Waisraeli. Tutaendelea mpaka tufike Gibea.”

Tazama sura Nakili




Waamuzi 19:12
9 Marejeleo ya Msalaba  

wamevuka kivuko; wamekwenda kulala katika Geba; Rama unatetemeka; Gibea wa Sauli umekimbia.


Pigeni tarumbeta katika Gibea, na baragumu katika Rama; pazeni sauti ya hofu katika Beth-aveni; nyuma yako, Ee Benyamini!


Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.


na Gibeoni, na Rama, na Beerothi;


na Zela, na Elefu, na huyo Myebusi (ndio Yerusalemu), na Gibeathi, na Kiriathi; miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake. Huo ndio urithi wa wana wa Benyamini kwa kufuata jamaa zao.


Basi hapo walipokuwa karibu na Yebusi, mchana ulikuwa umeendelea mno; yule mtumishi akamwambia bwana wake, Haya, tafadhali, tuende kando na kuingia mji huu wa Wayebusi, tulale humu.


Kisha akamwambia mtumishi wake, Haya, tuifikie miji hii mmojawapo nasi tutalala katika Gibea au katika Rama.


Sauli naye akaenda nyumbani kwake huko Gibea; na pamoja naye wakaenda kikosi cha watu, ambao Mungu alikuwa ameigusa mioyo yao.


Naye Sauli alijichagulia watu elfu tatu wa Israeli; ambao katika hao, elfu mbili walikuwa pamoja na Sauli katika Mikmashi, na katika mlima wa Betheli na elfu moja pamoja na Yonathani katika Gibea ya Benyamini; nao wale watu waliosalia akawaruhusu waende kila mtu hemani kwake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo