Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 17:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

2 Naye akamwambia mama yake, Hizo fedha elfu na mia moja ulizoibiwa, na kuweka laana kwa ajili yake na kusema masikioni mwangu, tazama, ninazo mimi hizo fedha; ni mimi niliyezitwaa. Mama yake akasema, Mwanangu na abarikiwe na BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Siku moja alimwambia mama yake, “Vile vipande 1,100 vya fedha ulivyoibiwa, nawe ukamlaani aliyekuibia nikisikia, mimi ninavyo. Mimi ndiye niliyevichukua.” Mama yake akasema, “Mwanangu, ubarikiwe na Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Siku moja alimwambia mama yake, “Vile vipande 1,100 vya fedha ulivyoibiwa, nawe ukamlaani aliyekuibia nikisikia, mimi ninavyo. Mimi ndiye niliyevichukua.” Mama yake akasema, “Mwanangu, ubarikiwe na Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Siku moja alimwambia mama yake, “Vile vipande 1,100 vya fedha ulivyoibiwa, nawe ukamlaani aliyekuibia nikisikia, mimi ninavyo. Mimi ndiye niliyevichukua.” Mama yake akasema, “Mwanangu, ubarikiwe na Mwenyezi-Mungu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Akamwambia mama yake, “Zile shekeli elfu moja na mia moja za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua.” Ndipo mama yake akamwambia, “Mwenyezi Mungu na akubariki, mwanangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Akamwambia mama yake, “Zile shekeli 1,100 za fedha zilizochukuliwa kwako, ambazo nilisikia ukizinenea maneno ya laana, hizi hapa; mimi ndiye niliyezichukua, lakini sasa ninakurudishia.” Ndipo mama yake akamwambia, “bwana na akubariki, mwanangu.”

Tazama sura Nakili




Waamuzi 17:2
21 Marejeleo ya Msalaba  

Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.


Nikagombana nao, nikawalaani, nikawapiga baadhi yao, na kuwang'oa nywele zao; nikawaapisha kwa Mungu, nikasema, Msiwaoze wana wao binti zenu, wala msiwatwae binti zao ili waolewe na wana wenu, wala na ninyi wenyewe.


Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.


Usilitaje bure jina la BWANA, Mungu wako, maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia mtu alitajaye jina lake bure.


Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa; Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.


Na alaaniwe mtu afanyaye kazi ya BWANA kwa ulegevu; na alaaniwe auzuiaye upanga wake usimwage damu.


Ndipo akaanza kulaani na kuapa akisema, Simjui mtu huyu. Na mara jogoo akawika.


Kwa maana ningeweza kuomba mimi mwenyewe niharimishwe na kutengwa na Kristo kwa ajili ya ndugu zangu, jamaa zangu kwa jinsi ya mwili;


Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha.


Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.


Maana yeye ampaye salamu azishiriki kazi zake mbovu.


Wakati huo alikuwako mtu mmoja wa nchi ya vilima ya Efraimu, aliyeitwa Mika.


Basi akamrudishia mama yake hizo fedha elfu na mia moja. Mama yake akasema, Mimi naziweka fedha hizi kabisa ziwe wakfu kwa BWANA, zitoke mkononi mwangu kwa ajili ya mwanangu, ili kufanya sanamu ya kuchonga, na sanamu ya kusubu; basi kwa hiyo nakurudishia wewe.


Ulaanini Merozi, alisema malaika wa BWANA, Walaanini kwa uchungu wenyeji wake; Kwa maana hawakuja kumsaidia BWANA, Kumsaidia BWANA juu ya hao wenye nguvu.


Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.


Nao watu wa Israeli walisumbuka sana siku ile; lakini Sauli alikuwa amewaapisha watu, akisema, Na alaaniwe mtu awaye yote alaye chakula chochote hadi jioni, nipate kujilipiza kisasi juu ya adui zangu. Basi hakuna mtu miongoni mwao aliyeonja chakula.


Ndipo mmojawapo wa watu akamjibu, akasema, Baba yako aliwaagiza watu sana kwa kiapo, akisema, Na alaaniwe mtu alaye chakula leo. Na hao watu walikuwa wamepungukiwa na nguvu.


Samweli akamwendea Sauli; naye Sauli akamwambia, Ubarikiwe na BWANA, nimeitimiza amri ya BWANA.


Naye Sauli akasema, Na mbarikiwe ninyi na BWANA; kwa sababu mmenihurumia.


Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo