Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 16:27 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

27 Basi nyumba ile ilikuwa imejaa wanaume kwa wanawake; na wakuu wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na juu ya dari palikuwa na watu elfu tatu wanaume kwa wanawake waliokuwa wakitazama, wakati Samsoni alipocheza.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Jumba hilo lilikuwa limejaa watu: Wakuu wote wa Wafilisti walikuwapo na kwenye paa kulikuwa na watu 3,000 wanaume na wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Jumba hilo lilikuwa limejaa watu: Wakuu wote wa Wafilisti walikuwapo na kwenye paa kulikuwa na watu 3,000 wanaume na wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Jumba hilo lilikuwa limejaa watu: wakuu wote wa Wafilisti walikuwapo na kwenye paa kulikuwa na watu 3,000 wanaume na wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Basi lile jengo lilikuwa na wanaume na wanawake wengi; viongozi wote wa Wafilisti walikuwa humo, na kwenye dari walikuwepo watu wapatao elfu tatu, wanaume kwa wanawake, wakimtazama Samsoni akiwatumbuiza.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Basi lile jengo lilikuwa na wingi wa watu waume kwa wake; viongozi wote wa Wafilisti walikuwamo humo, na kwenye sakafu ya juu walikuwepo watu 3,000 waume kwa wake, waliokuwa wakimtazama Samsoni wakati anacheza.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 16:27
6 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.


Utakapojenga nyumba mpya, fanya ukuta kandokando ya dari lako, usije ukaleta damu juu ya nyumba yako, mtu akianguka huko.


Tena kabla hawajalala akawaendea juu darini,


Samsoni akamwambia yule kijana aliyemshika mkono, Niache nizipapase nguzo ambazo nyumba hii inazikalia, nipate kuzitegemea.


Samsoni akamwita BWANA, akasema, Ee Bwana MUNGU, nikumbuke nakuomba, ukanitie nguvu, nakuomba, mara hii tu, Ee Mungu, ili nipate kujilipiza kisasi juu ya Wafilisti kwa ajili ya macho yangu mawili.


Lakini ndani ya huo mji palikuwa na mnara wenye nguvu, na watu wote wanaume na wanawake wakakimbilia huko, na watu wote wa mji, nao wakajifungia ndani, wakapanda paa la mnara.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo