Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 16:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Naye akamlaza usingizi magotini pake. Kisha akamwita mtu akavinyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake; akaanza kumsumbua, nguvu zake zikamtoka.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Naye Delila akamfanya Samsoni alale usingizi magotini mwake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi vyake saba. Kisha Delila akaanza kumtesa Samsoni kwa kuwa sasa nguvu zilikuwa zimemtoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Naye Delila akamfanya Samsoni alale usingizi magotini mwake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi vyake saba. Kisha Delila akaanza kumtesa Samsoni kwa kuwa sasa nguvu zilikuwa zimemtoka.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Naye Delila akamfanya Samsoni alale usingizi magotini mwake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi vyake saba. Kisha Delila akaanza kumtesa Samsoni kwa kuwa sasa nguvu zilikuwa zimemtoka.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Delila akamfanya alale usingizi magotini pake, akamwita mtu amnyoe vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake. Delila akaanza kumnyong’onyesha Samsoni, nazo nguvu zake zikamtoka.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Delila akamfanya alale usingizi magotini pake, akamwita mtu akamnyoa vile vishungi saba vya nywele za kichwa chake. Akaanza kumsumbua ili aamke nazo nguvu zake zikamtoka.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 16:19
6 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti; yaani, mwanamke ambaye moyo wake ni mitego na tanzi, na mikono yake ni kama vifungo; yeye ampendezaye Mungu atamponyoka, bali mwenye dhambi atanaswa na yeye.

Delila alipoona ya kuwa amemwambia yote yaliyokuwa moyoni mwake, akatuma mtu akawaita wakuu wa Wafilisti, akisema, Njoni huku mara hii tu, maana ameniambia siri yake yote. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakamwendea wakachukua ile fedha mikononi mwao.

Kisha akasema, Samsoni, Wafilisti wanakujia. Akaamka katika usingizi wake, akasema, Nitakwenda nje kama siku nyingine, na kujinyosha. Lakini hakujua ya kuwa BWANA amemwacha.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo