Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 15:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Lakini Mungu akapasua mahali penye shimo palipo katika Lehi, pakatoka maji; naye alipokunywa, roho yake ikamrudia, akaburudika; kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Enhakore, napo pa katika Lehi hata hivi leo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mungu akafungua mahali palipokuwa na shimo huko Leki, akatiririsha maji. Samsoni akanywa maji hayo na nguvu zake zikamrudia. Chemchemi hiyo ikaitwa En-hakore; nayo iko huko Lehi mpaka leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Ndipo Mungu akafunua shimo huko Lehi, na maji yakatoka. Samsoni alipoyanywa maji hayo, nguvu zikamrudia, akahuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko hadi leo huko Lehi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 bwana akafunua shimo huko Lehi, pakatoka maji. Samsoni alipoyanywa, nguvu zikamrudia na kuhuika. Hivyo chemchemi ile ikaitwa En-Hakore, nayo iko mpaka leo huko Lehi.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 15:19
16 Marejeleo ya Msalaba  

Akampa jina BWANA aliyesema naye, “Wewe U Mungu uonaye,” kwani alisema, “Kweli nimemwona Mungu na nikaendelea kuishi baada ya kumuona?”


Akaita jina la mahali pale Betheli; lakini jina la mji ule hapo kwanza uliitwa Luzu.


Maana mali yako ilikuwa haba kabla sijaja, nayo imezidi kuwa nyingi, BWANA akakubariki kila nilikokwenda. Basi sasa, nitaangalia lini mambo ya nyumba yangu mwenyewe?


Wakamwambia maneno yote ya Yusufu, aliyowaambia; na alipoona magari aliyotuma Yusufu, ili kumchukua, roho ya Yakobo baba yao ikafufuka.


Atakunywa maji ya mto njiani; Kwa hiyo atakiinua kichwa chake kwa ushindi.


Katika shida yangu nilimlilia BWANA Naye akaniitikia.


Maskini huyu aliita, BWANA akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Musa akajenga madhabahu, akaiita jina lake Yahweh-nisi;


Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.


Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.


Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;


Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.


Basi Wafilisti wakapanda wakapiga kambi yao katika Yuda, wakashambulia Lehi.


kisha wakampa kipande cha mkate wa tini, na vishada viwili vya zabibu; naye akiisha kula roho yake ikamrudia; kwa maana hakuwa amekula chakula wala kunywa maji, siku tatu mchana na usiku.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo