Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 15:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Wakamwambia, Tumeshuka ili kukufunga, tupate kukutia katika mikono ya Wafilisti. Samsoni akawaambia, Niapieni ya kwamba ninyi wenyewe hamtaniua.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga ili tukutie mikononi mwao.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba nyinyi wenyewe hamtaniua.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga ili tukutie mikononi mwao.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba nyinyi wenyewe hamtaniua.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga ili tukutie mikononi mwao.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kwamba nyinyi wenyewe hamtaniua.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Wakamwambia, “Tumekuja kukufunga na kukutia mikononi mwa Wafilisti.” Samsoni akawaambia, “Niapieni kuwa hamtaniua ninyi wenyewe.”

Tazama sura Nakili

Waamuzi 15:12
7 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme Sulemani akatuma kuwa jambo hilo liwe mkononi mwa Benaya mwana wa Yehoyada: naye akampiga, hata akafa.

Ndipo Benaya, mwana wa Yehoyada, akapanda, akampiga, akamwua; naye akazikwa katika nyumba yake mwenyewe iliyoko nyikani.

wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa mtawala.

Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovu kwa mkono wake, lakini hawakufahamu.

Ndipo watu elfu tatu wa Yuda wakateremka hadi katika ule ufa wa jabali la Etamu, wakamwambia Samsoni, Je! Hujui ya kuwa Wafilisti wanatutawala? Ni nini hii, basi, uliyotutenda? Akawaambia, Kadiri ile walivyonitenda mimi, ndivyo nilivyowatenda wao.

Wakamwambia, wakisema, Vema, lakini tutakufunga sana, na kukutia katika mikono yao; lakini hakika hatutakuua. Basi wakamfunga kwa kamba mbili mpya, wakamchukua kutoka huko jabalini.

Ndipo hapo Zeba na Salmuna wakasema, Simama wewe utuue sisi; kwa maana kama mtu alivyo, ndivyo zilivyo nguvu zake. Basi Gideoni akasimama, akawaua Zeba na Salmuna, akazitwaa koja zilizokuwa katika shingo za ngamia wao.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo