Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 14:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Akatwaa asali mikononi mwake akasonga mbele, huku akila alipokuwa akienda, akawafikia babaye na mamaye, akawapa, nao wakala; lakini hakuwaambia ya kuwa ameitwaa hiyo asali katika mzoga wa simba.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakala. Lakini hakuwaambia kwamba alitoa asali hiyo ndani ya mzoga wa simba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakala. Lakini hakuwaambia kwamba alitoa asali hiyo ndani ya mzoga wa simba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Basi, akapakua asali kwa mikono yake akawa anakula huku akiendelea na safari yake. Aliporudi kwa wazazi wake, akawapa asali kidogo nao wakala. Lakini hakuwaambia kwamba alitoa asali hiyo ndani ya mzoga wa simba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Akachukua asali mkononi mwake, akala huku akitembea. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa kiasi cha ile asali, nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa aliitwaa asali katika mzoga wa simba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 akachukua asali mkononi mwake akaendelea huku akila. Alipowafikia baba yake na mama yake, akawapa ile asali nao wakala. Lakini hakuwaambia kuwa alitwaa asali kutoka kwenye mzoga wa simba.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 14:9
7 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanangu, ule asali, kwa maana ni njema, Na sega la asali lililo tamu ulionjapo.

Kwa uvumilivu mwingi mkuu husadikishwa; Na ulimi laini huvunja mfupa.

Basi babaye akamteremkia huyo mwanamke; Samsoni naye akafanya karamu huko; kwa kuwa ndivyo vijana walivyokuwa wakifanya.

Kisha baadaye akarudi ili kumtwaa, naye akaenda kando kuuangalia mzoga wa huyo simba; na tazama, nyuki wengi walikuwamo ndani ya mzoga wa simba, na asali.

Lakini Sauli akamjibu babaye mdogo, Alituambia waziwazi ya kuwa hao punda wamekwisha onekana. Lakini habari ya ufalme, ambayo Samweli alimwambia, hakuitaja.

Basi ikatukia siku moja, ya kwamba Yonathani, mwana wa Sauli, akamwambia yule kijana aliyembebea silaha zake, Haya! Na tuvuke twende kwa Wafilisti ngomeni, pale ng'ambo ya pili. Lakini hakumwarifu babaye.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo