Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 14:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Roho ya BWANA ikamjia juu yake kwa nguvu, naye akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavazi hayo ya sikukuu. Hasira zake zikampanda, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Hapo roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu, naye akaenda mjini Ashkeloni, akawaua watu thelathini, kisha akachukua mavazi yao ya sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda nyumbani kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Hapo roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu, naye akaenda mjini Ashkeloni, akawaua watu thelathini, kisha akachukua mavazi yao ya sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda nyumbani kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Hapo roho ya Mwenyezi-Mungu ikamjia Samsoni kwa nguvu, naye akaenda mjini Ashkeloni, akawaua watu thelathini, kisha akachukua mavazi yao ya sikukuu, akawapa wale waliotegua kitendawili chake. Halafu akaondoka, akaenda nyumbani kwa wazazi wake akiwa na hasira kali.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Ndipo Roho wa Mwenyezi Mungu akamjia Samsoni kwa nguvu. Samsoni akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini wa mji huo, akatwaa mali yao, akawapa watu wale waliotegua kile kitendawili nguo zao. Akiwa amejaa hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Ndipo Roho wa bwana akamjia Samsoni kwa nguvu. Akateremka mpaka Ashkeloni, akawaua watu waume thelathini miongoni mwa watu wa mji, akatwaa mali zao na nguo zao, akawapa watu wale waliofumbua kile kitendawili. Akiwa na hasira, akakwea kurudi nyumbani kwa baba yake.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 14:19
9 Marejeleo ya Msalaba  

Pamoja na haya Yuda aliutwaa Gaza pamoja na mipaka yake, na Ashkeloni na mipaka yake, na Ekroni na mipaka yake.


Roho ya BWANA ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.


Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu.


Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, naye akampasua kana kwamba anampasua mwana-mbuzi, wala hakuwa na kitu chochote mkononi mwake; lakini hakuwaambia baba yake na mama yake aliyoyafanya.


Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.


Roho ya BWANA ikamjia juu yake, naye akawa mwamuzi wa Israeli; akatoka kuenda vitani, naye BWANA akamtia huyo Kushan-rishathaimu, mfalme wa Mesopotamia, mkononi mwake; na mkono wake ukamshinda Kushan-rishathaimu.


Na Roho ya Mungu ikamjia Sauli kwa nguvu, hapo alipoyasikia maneno yale, na hasira yake ikawaka sana.


Hii ndiyo hesabu ya yale majipu waliyoyapeleka wale Wafilisti, yawe matoleo ya kosa kwa BWANA; kwa Ashdodi moja, kwa Gaza moja, kwa Ashkeloni moja, kwa Gathi moja, na kwa Ekroni moja;


Ndipo wakauliza, Na hayo matoleo ya kosa tutakayompelekea, yatakuwa ya namna gani? Na yawe majipu ya dhahabu matano, na panya wa dhahabu watano, sawasawa na idadi ya wakuu wa Wafilisti; kwa kuwa tauni moja ilikuwa juu yenu nyote, na juu ya wakuu wenu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo