Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 14:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Naye akalia mbele yake hizo siku saba, wakati ulioendelea karamu yao; basi ikawa siku ya saba akamwambia, kwa sababu alikuwa akimsisitiza sana; naye akawaambia wale wana wa watu wake hicho kitendawili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za harusi. Siku ya saba Samsoni akamwambia mkewe kile kitendawili kwani alimbana sana. Mkewe akaenda haraka akawaambia watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za harusi. Siku ya saba Samsoni akamwambia mkewe kile kitendawili kwani alimbana sana. Mkewe akaenda haraka akawaambia watu wake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Lakini aliendelea kulia katika muda wao wote wa siku saba za sherehe za harusi. Siku ya saba Samsoni akamwambia mkewe kile kitendawili kwani alimbana sana. Mkewe akaenda haraka akawaambia watu wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye mkewe akawaeleza watu wake kile kitendawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Mkewe akalia kwa muda wa zile siku zote saba za karamu. Hivyo siku ile ya saba Samsoni akamweleza, kwa kuwa aliendelea kumsisitiza sana. Naye akawaeleza watu wake kile kitendawili.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 14:17
13 Marejeleo ya Msalaba  

Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alichuma matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.


Ndipo mkewe akamwambia, Je! Wewe hata sasa washikamana na utimilifu wako? Mkufuru Mungu, ufe.


Kwa maneno yake mengi na ulaini akamshawishi, Kwa ubembelezi wa midomo yake akamshinda.


Huupinda ulimi wao, kana kwamba ni upinde, ili kusema uongo; nao wamepata nguvu katika nchi, lakini si katika uaminifu; maana huendelea toka ubaya hata ubaya, wala hawanijui mimi, asema BWANA.


Msimwamini rafiki, msimwekee kiongozi tumaini; ilinde milango ya midomo ya kinywa chako ili mkeo alalaye kifuani mwako asijue habari.


Nawaambia ya kwamba, ijapokuwa hatoki ampe kwa kuwa ni rafiki yake, lakini kwa vile asivyoacha kumwomba, atatoka na kumpa kadiri ya haja yake.


Basi mkewe Samsoni akalia mbele yake, akasema, Wewe wanichukia tu, wala hunipendi; wewe umewategea kitendawili hao wana wa watu wangu, nawe hukuniambia mimi. Naye akamwambia, Angalia, sikumwambia baba yangu wala mama yangu, mbonai nikuambie wewe?


Nao watu wa mji wakamwambia siku ya saba kabla ya jua kuchwa, Ni kitu gani kilicho tamu kuliko asali? Ni kitu gani kilicho na nguvu kuliko simba? Naye akawaambia, Msingelima na mtamba wangu, Hamngekitegua kitendawili changu.


Delila akamwambia Samsoni, Hata sasa umenidhihaki, umenidanganya; niambie sasa, waweza kufungwa kwa kitu gani? Akamwambia, Ukivifuma hivi vishungi saba vya nywele za kichwa changu katika mtande wa nguo.


Hatimaye, kwa vile alivyomsumbua kwa maneno yake kila siku, na kumuudhi, roho yake ikataabika karibu kufa.


Delila akamwambia Samsoni, Tafadhali niambie asili ya nguvu zako nyingi, na jinsi uwezavyo kufungwa, ili uteswe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo