Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 14:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Naye akawaambia, Kutoka kwa huyo kikatoka chakula, Kutoka kwa huyo mwenye nguvu kikatoka kitamu. Nao katika siku tatu hawakuweza kukifumbua hicho kitendawili.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Nao wakamwambia, “Haya tega tusikie.” Samsoni akawaambia, “Kwa mla kukatoka mlo kwa mwenye nguvu, utamu.” Baada ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Nao wakamwambia, “Haya tega tusikie.” Samsoni akawaambia, “Kwa mla kukatoka mlo kwa mwenye nguvu, utamu.” Baada ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Nao wakamwambia, “Haya tega tusikie.” Samsoni akawaambia, “Kwa mla kukatoka mlo kwa mwenye nguvu, utamu.” Baada ya siku tatu hao vijana walikuwa bado hawajaweza kutegua hicho kitendawili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 Akawaambia, “Ndani ya mlaji, kulitoka kitu cha kuliwa, ndani ya mwenye nguvu, kulitoka kitu kitamu.” Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 Akawaambia, “Ndani ya mlaji, kulitoka kitu cha kuliwa, ndani ya mwenye nguvu, kulitoka kitu kitamu.” Kwa muda wa siku tatu hawakuweza kutoa jibu.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 14:14
20 Marejeleo ya Msalaba  

nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.

Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio Engedi).

Nao Yehoshafati na watu wake walipokuja kuchukua nyara zao, wakakuta miongoni mwao mifugo wengi sana, mali, mavazi na vitu vya thamani, walivyojinyakulia, zaidi kuliko wawezavyo kuchukua; wakawa siku tatu katika kuteka nyara, maana zilikuwa nyingi sana.

Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni.

Akajibu, akawaambia, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa mbinguni, bali wao hawakujaliwa.

Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye.

Lakini katika mambo hayo yote sisi ni zaidi ya washindi, kupitia kwake yeye aliyetupenda.

Maana dhiki yetu nyepesi, iliyo ya muda mfupi tu, yatuandalia utukufu wa milele uzidio kuwa mwingi sana;

Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.

lakini msipoweza kunitegulia ndipo mtakaponipa mimi mavazi thelathini ya kitani na mavazi thelathini ya sikukuu. Basi wakamwambia, Haya, tega kitendawili chako, ili tupate kukisikia.

Ikawa kwa siku ya saba, wakamwambia mkewe Samsoni, Mbembeleze mumeo, ili atutegulie hicho kitendawili, tusije tukakuteketeza moto wewe na nyumba ya baba yako; je! Mmetuita ili mpate kuichukua mali yetu? Je! Sivyo?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo