Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 13:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Lakini malaika wa BWANA akamwambia Manoa, “Ijapokuwa unanizuia, sitakula chakula chako; lakini kama unataka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, inakupasa kumsogezea BWANA”. Kwa kuwa Manoa hakujua ya kwamba yeye ni malaika wa BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Hata kama mkinilazimisha kukaa sitakula chakula chenu. Lakini kama ukipenda, tayarisha sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi-Mungu.” Manoa hakujua kuwa huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Yule malaika wa Mwenyezi-Mungu akamwambia Manoa, “Hata kama mkinilazimisha kukaa sitakula chakula chenu. Lakini kama ukipenda, tayarisha sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi-Mungu.” Manoa hakujua kuwa huyo alikuwa malaika wa Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Malaika wa Mwenyezi Mungu akamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula chochote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtolee Mwenyezi Mungu.” (Manoa hakumtambua kuwa huyu alikuwa malaika wa Mwenyezi Mungu.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Malaika wa bwana akamjibu, “Hata kama utanizuia, sitakula chochote kwako. Lakini ukitaka kuandaa sadaka ya kuteketezwa, mtolee bwana hiyo sadaka.” (Kwa kuwa Manoa hakujua kuwa alikuwa malaika wa bwana.)

Tazama sura Nakili

Waamuzi 13:16
5 Marejeleo ya Msalaba  

Nami nitaleta chakula kidogo, mkaburudishe moyo, baadaye mwendelee, kwa maana mmemjia mtumwa wenu. Wakasema, Haya, fanya kama ulivyosema.

Lakini malaika wa BWANA hakumtokea Manoa tena, wala mkewe. Ndipo Manoa alipojua ya kwamba ndiye malaika wa BWANA.

Lakini mkewe akamwambia, Kama BWANA angetaka kutuua hangepokea sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, mikononi mwetu, wala hangetuonesha mambo hayo yote, wala hangetuambia mambo kama hayo wakati huu.

Naye malaika wa Mungu akamwambia, Itwae nyama na mikate isiyotiwa chachu, uiweke juu ya mwamba huu, ukaumwage huu mchuzi. Akafanya hivyo.

ukamjengee BWANA, Mungu wako, madhabahu juu ya ngome hii, kwa taratibu zake; ukamtwae yule ng'ombe wa pili na kumtoa awe sadaka ya kuteketezwa, kwa kuni za ile Ashera uliyoikata.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo