Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 11:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

39 Basi ikawa mwisho wa hiyo miezi miwili, akarudi kwa babaye, aliyemtenda sawasawa na ile nadhiri yake aliyokuwa ameiweka; naye alikuwa hajamjua mwanamume. Kisha ikawa desturi katika Israeli,

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

39 Baada ya miezi miwili akarudi nyumbani; kisha baba yake akamtendea kulingana na nadhiri yake. Msichana huyo hakuwa amemjua mwanamume yeyote. Basi, tangu wakati huo kukawa na desturi hii katika Israeli:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

39 Baada ya miezi miwili akarudi nyumbani; kisha baba yake akamtendea kulingana na nadhiri yake. Msichana huyo hakuwa amemjua mwanamume yeyote. Basi, tangu wakati huo kukawa na desturi hii katika Israeli:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

39 Baada ya miezi miwili akarudi nyumbani; kisha baba yake akamtendea kulingana na nadhiri yake. Msichana huyo hakuwa amemjua mwanamume yeyote. Basi, tangu wakati huo kukawa na desturi hii katika Israeli:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

39 Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba yake, naye baba yake akamtendea kama alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa bikira. Nayo ikawa desturi katika Israeli,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

39 Baada ya hiyo miezi miwili, alirejea kwa baba yake, naye baba yake akamtendea kama alivyokuwa ametoa nadhiri yake. Naye alikuwa bikira. Nayo ikawa desturi katika Israeli,

Tazama sura Nakili

Waamuzi 11:39
12 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Yeremia akamlilia Yosia; na waimbaji wote wanaume kwa wawanawake wakamtaja Yosia katika maombolezo yao, hadi leo; hata wakayafanya kuwa ada kwa Israeli; nayo, tazama, yameandikwa katika Maombolezo.

Yeye achinjaye ng'ombe ni kama yeye amwuaye mtu; na yeye atoaye dhabihu ya mwana-kondoo ni kama yeye avunjaye shingo ya mbwa; na yeye atoaye matoleo ni kama yeye atoaye damu ya nguruwe; na yeye afukizaye uvumba ni kama yeye abarikiye sanamu; naam, wamezichagua njia zao wenyewe, na nafsi zao zafurahia machukizo yao.

Usimtende kama haya BWANA, Mungu wako; kwani kila yaliyo machukizo kwa BWANA, ayachukiayo yeye, wameifanyia miungu yao; kwa maana hata wana wao na binti zao huiteketezea hiyo miungu yao ndani ya moto.

ndipo itakuwa ya kwamba, kile kitakachotoka katika milango ya nyumba yangu kunilaki, hapo nitakaporudi na ushindi kutoka kwa hao wana wa Amoni, kitu hicho kitakuwa ni cha BWANA, nami nitakisongeza kiwe sadaka ya kuteketezwa.

Akamwambia, Haya, nenda. Akampeleka mbali muda wa miezi miwili; naye akaenda zake, yeye na wenziwe, akauombolea ubikira wake huko milimani.

kwamba binti za Israeli waende mwaka baada ya mwaka ili kumkumbuka huyo mwana wa Yeftha, Mgileadi, siku nne katika mwaka.

Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.

Bali Hana hakukwea; maana alimwambia mumewe, Sitakwea mimi hata mtoto wangu atakapoachishwa kunyonya, hapo ndipo nitakapomleta, ili awepo mbele za BWANA, akae huko daima.

Naye alipomwachisha kunyonya, akamchukua pamoja naye, na ng'ombe watatu, na efa moja ya unga, na chupa ya divai, akamleta nyumbani kwa BWANA, huko Shilo; na yule mtoto alikuwa mtoto mdogo.

kwa sababu hiyo mimi nami nimempa BWANA mtoto huyu; wakati wote atakaokuwa hai amepewa BWANA. Naye akamwabudu BWANA huko.

Lakini Samweli alikuwa akitumika mbele za BWANA, naye alikuwa kijana aliyevaa naivera ya kitani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo