Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 11:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 BWANA, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawapiga; basi Israeli wakaimiliki hiyo nchi ya Waamori, waliokaa katika nchi hiyo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni pamoja na watu wake mikononi mwa Waisraeli, wakawashinda. Hivyo Waisraeli wakachukua nchi yote ya Waamori ambao walikuwa wanaishi huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni pamoja na watu wake mikononi mwa Waisraeli, wakawashinda. Hivyo Waisraeli wakachukua nchi yote ya Waamori ambao walikuwa wanaishi huko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni pamoja na watu wake mikononi mwa Waisraeli, wakawashinda. Hivyo Waisraeli wakachukua nchi yote ya Waamori ambao walikuwa wanaishi huko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “Ndipo Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Waisraeli, nao wakawashinda. Waisraeli wakaimiliki nchi yote ya Waamori walioishi nchi hiyo,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “Ndipo bwana, Mungu wa Israeli, akamtia Sihoni na watu wake wote mikononi mwa Israeli, nao wakawashinda. Israeli wakaitwaa nchi yote ya Waamori, waliokuwa wakiishi katika nchi hiyo,

Tazama sura Nakili




Waamuzi 11:21
8 Marejeleo ya Msalaba  

Wana wa Israeli wakakimbia mbele ya Yuda; naye Mungu akawaua mikononi mwao.


je! Haikuwapasa kujua ya kwamba BWANA, Mungu wa Israeli, alimpa Daudi ufalme juu ya Israeli milele, yeye na wanawe kwa agano la chumvi?


Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.


Lakini nilimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini niliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.


Israeli wakampiga kwa makali ya upanga, na kuimiliki nchi yake, tangu mto wa Arnoni hata mto wa Yaboki, mpaka nchi ya wana wa Amoni; kwa kuwa mpaka wa wana wa Amoni ulikuwa una nguvu.


Ndipo Sihoni alipojitokeza juu yetu, yeye na watu wake wote ili kupigana nasi huko Yahasa.


BWANA akamwambia Yoshua, Tazama, nimeutia Yeriko katika mkono wako, na mfalme wake, na mashujaa wake.


Lakini huyo Sihoni hakuwaamini Israeli ili wapite ndani ya mpaka wake; bali Sihoni akawakutanisha watu wake wote, nao wakapiga kambi katika Yahasa, wakapigana na Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo