Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 11:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Kisha akaenda nyikani na kuizunguka hiyo nchi ya Edomu, na nchi ya Moabu, nao wakapita upande wa mashariki mwa nchi ya Moabu, wakapiga kambi upande wa pili wa Arnoni; wala hawakuingia ndani ya mpaka wa Moabu, kwa maana Arnoni ilikuwa ni mpaka wa Moabu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kisha wakasafiri wakipitia jangwani kuzunguka nchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ngambo ya mto Arnoni. Lakini hawakuingia eneo la Moabu. Mto Arnoni ndio uliokuwa mpaka wa Moabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kisha wakasafiri wakipitia jangwani kuzunguka nchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ngambo ya mto Arnoni. Lakini hawakuingia eneo la Moabu. Mto Arnoni ndio uliokuwa mpaka wa Moabu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kisha wakasafiri wakipitia jangwani kuzunguka nchi ya Edomu na Moabu mpaka walipofika upande wa mashariki wa Moabu, wakapiga kambi ng'ambo ya mto Arnoni. Lakini hawakuingia eneo la Moabu. Mto Arnoni ndio uliokuwa mpaka wa Moabu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 “Baadaye wakasafiri kupitia jangwa, wakiambaa na nchi za Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu, na kupiga kambi upande ule mwingine wa Mto Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Mto Arnoni ulikuwa mpaka wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 “Baadaye wakasafiri kupitia jangwa, wakiambaa na nchi za Edomu na Moabu, wakapitia upande wa mashariki wa nchi ya Moabu na kupiga kambi upande mwingine wa Arnoni. Hawakuingia katika nchi ya Moabu, kwa kuwa Arnoni ilikuwa mpaka wake.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 11:18
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha wakasafiri kutoka Kadeshi; wana wa Israeli, mkutano mzima, wakafikia mlima wa Hori.


Balaki aliposikia ya kuwa Balaamu amefika, akatoka kwenda kumlaki, mpaka Mji wa Moabu, ulioko katika mpaka wa Arnoni, ulioko katika upande wa mwisho wa mpaka huo.


Hivi leo ivuke Ari, mpaka wa Moabu;


Ondokeni, mshike safari yenu, mvuke bonde la Arnoni; tazama, nimemtia Sihoni Mwamori mfalme wa Heshboni mkononi mwako, na nchi yake; anzeni kuimiliki, mshindane naye katika mapigano.


BWANA akaniambia, Usiwasumbue Wamoabi, wala usishindane nao katika mapigano; kwa kuwa sitakupa katika nchi yake kuimiliki; kwa sababu Ari nimewapa wana wa Lutu kuimiliki.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo