Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Waamuzi 11:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 lakini hapo walipokwea kutoka Misri, na Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu, na Kadeshi;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Lakini Waisraeli walipotoka Misri, walisafiri jangwani hadi bahari ya Shamu mpaka Kadeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Lakini Waisraeli walipotoka Misri, walisafiri jangwani hadi bahari ya Shamu mpaka Kadeshi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Lakini Waisraeli walipotoka Misri, walisafiri jangwani hadi bahari ya Shamu mpaka Kadeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Lakini walipopanda kutoka Misri, Waisraeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu na wakafika Kadeshi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Lakini walipopanda kutoka Misri, Israeli walipitia katika jangwa hadi Bahari ya Shamu na wakafika Kadeshi.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 11:16
9 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.


Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonesha matunda ya nchi.


Basi Mwamaleki na Mkanaani wakaa katika bonde; kesho geukeni, mkaende jangwani kwa njia iendayo Bahari ya Shamu.


Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia jangwa la Sinai, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko.


Mbona mmewaleta kusanyiko la BWANA hadi jangwani hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu?


Na ninyi basi geukeni, mshike safari yenu, mwende jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu.


Ndipo mkakaa Kadeshi siku nyingi, kwa kadiri ya hizo siku mlizokaa.


Kwa kuwa wana wa Israeli walitembea muda wa miaka arubaini barani, hadi hilo taifa zima, yaani, watu wanaume wapiganaji vita, waliotoka Misri, walipokuwa wameangamia; kwa sababu hawakuisikiza sauti ya BWANA; nao ndio BWANA aliowaapia ya kwamba hatawaacha waione hiyo nchi, ambayo BWANA aliwaapia baba zao kwamba atatupa sisi; nchi itiririkayo maziwa na asali.


akamwambia, Yeftha anakuambia hivi; Israeli hakuitwaa nchi ya Moabu, wala nchi ya wana wa Amoni;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo