Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 10:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Na hao watu, wakuu wa Gileadi, wakaambiana wao kwa wao, Je! Ni mtu yupi atakayeanza kupigana na wana wa Amoni? Yeye atakuwa ni kichwa juu ya wenyeji wote wa Gileadi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Waisraeli na viongozi wao wakaulizana, “Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Atakayefanya hivyo ndiye atakayekuwa kiongozi wa wakazi wote wa Gileadi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Waisraeli na viongozi wao wakaulizana, “Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Atakayefanya hivyo ndiye atakayekuwa kiongozi wa wakazi wote wa Gileadi.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Waisraeli na viongozi wao wakaulizana, “Ni nani atakayeanza kupigana na Waamoni? Atakayefanya hivyo ndiye atakayekuwa kiongozi wa wakazi wote wa Gileadi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana wao kwa wao, “Yeyote atakayeanzisha mashambulizi dhidi ya Waamoni atakuwa kiongozi wa wote wanaoishi Gileadi.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Viongozi wa watu wa Gileadi wakaambiana wao kwa wao, “Yeyote yule atakayeanzisha mashambulizi dhidi ya Waamoni atakuwa kiongozi wa wote wakaao Gileadi.”

Tazama sura Nakili




Waamuzi 10:18
10 Marejeleo ya Msalaba  

Watawaitia wakuu wake ufalme, lakini hawatakuwapo; wakuu wake wote wamekuwa si kitu.


Ikawa baada ya kufa kwake Yoshua, wana wa Israeli wakamwuliza BWANA, wakisema, Ni nani atakayekwea kwanza kwa ajili yetu juu ya Wakanaani, ili kupigana nao?


Wakati huo wana wa Amoni walikutana pamoja, wakapiga kambi huko Gileadi. Wana wa Israeli nao wakajikusanya wakapiga kambi Mispa.


Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu shujaa sana, naye alikuwa ni mwana wa mwanamke kahaba; Gileadi akamzaa Yeftha.


Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kiongozi, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya BWANA huko Mispa.


Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli.


Huyo Yeftha akawa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka sita. Ndipo akafa Yeftha, Mgileadi, akazikwa katika miji ya Gileadi mmojawapo.


Watu wa Israeli wakasema, Je! Mmemwona mtu huyu aliyepanda huko? Hakika ametokea ili awatukane Israeli; basi, itakuwa, mtu yule atakayemwua, mfalme atampa utajiri mwingi, naye atamwoza binti yake, na kuufanya ukoo wa baba yake kuwa huru katika Israeli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo