Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 10:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Wakati huo wana wa Amoni walikutana pamoja, wakapiga kambi huko Gileadi. Wana wa Israeli nao wakajikusanya wakapiga kambi Mispa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Waamoni wakajikusanya wakapiga kambi yao huko Gileadi. Waisraeli nao wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Mizpa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Waamoni wakajikusanya wakapiga kambi yao huko Gileadi. Waisraeli nao wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Mizpa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Waamoni wakajikusanya wakapiga kambi yao huko Gileadi. Waisraeli nao wakakusanyika na kupiga kambi yao huko Mizpa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Waamoni walipoitwa vitani na kupiga kambi kule Gileadi, Waisraeli walikusanyika na kupiga kambi huko Mispa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Ndipo Waamoni wakaitwa vitani na kupiga kambi huko Gileadi, Waisraeli wakakusanyika na kupiga kambi huko Mispa.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 10:17
9 Marejeleo ya Msalaba  

na Mispa, maana alisema, Mungu avizie kati ya mimi na wewe, wakati tusipoonana.


tena kutoka Heshboni mpaka Ramath-Mizpe, na Betonimu; tena kutoka Mahanaimu hadi mpaka wa Debiri;


Na hao watu, wakuu wa Gileadi, wakaambiana wao kwa wao, Je! Ni mtu yupi atakayeanza kupigana na wana wa Amoni? Yeye atakuwa ni kichwa juu ya wenyeji wote wa Gileadi.


Ndipo Yeftha akaenda pamoja na wazee wa Gileadi, na hao watu wakamfanya awe kiongozi, tena mkuu, juu yao; naye Yeftha akanena maneno yake yote mbele ya BWANA huko Mispa.


Ndipo Roho ya BWANA ikamjia Yeftha, naye akapita katika Gileadi na Manase, akapita na katika Mispa ya Gileadi, na kutoka hapo Mispa ya Gileadi akapita kuwaendea wana wa Amoni.


Kisha Yeftha akafika Mispa nyumbani kwake, na tazama, binti yake akamtokea kumlaki, na matari na akichezacheza; naye alikuwa ni mwanawe wa pekee; hakuwa na mwingine, wa kiume wala binti.


Ikawa baadaye, wana wa Amoni wakapigana na Israeli.


wakamwambia Yeftha, Njoo wewe uwe kichwa chetu, ili tupate kupigana na wana wa Amoni.


Samweli akasema, Wakusanyeni Waisraeli wote Mispa, nami nitawaombea ninyi kwa BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo