Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Waamuzi 1:35 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

35 lakini hao Waamori waliendelea kukaa katika kilima cha Heresi, na katika Aiyaloni, na katika Shaalbimu; pamoja na haya mkono wa hiyo nyumba ya Yusufu ulishinda, hata wakawalazimisha shokoa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 Waamori waliendelea kuishi katika miji iliyokuwa katika kilima cha Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu. Lakini watu wa makabila ya Manase na Efraimu waliwatawala Waamori na kuwafanya wafanye kazi za kulazimishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Waamori pia walikuwa wameamua kuendelea kuishi katika Mlima Heresi, Aiyaloni na Shaalbimu; lakini nguvu ya nyumba ya Yusufu ilipoongezeka, wao pia wakashindwa na wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Waamori pia wakaendelea kukaa katika Mlima Heresi, katika Aiyaloni na Shaalbimu, lakini mkono wa nyumba ya Yusufu ukawalemea, nao wakashindwa hata wakalazimika kuingia katika kazi ya kulazimishwa.

Tazama sura Nakili

Waamuzi 1:35
8 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Beth-shemeshi na Elon-beth-hanani.

watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.

Ndipo Yoshua akanena na BWANA katika siku hiyo ambayo BWANA aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israeli; akasema mbele ya macho ya Israeli, Wewe Jua, simama kimya juu ya Gibeoni; Na wewe Mwezi, simama katika bonde la Aiyaloni.

Shaalabini, Aiyaloni, Ithla;

Eloni, Timna, Ekroni;

Kisha Waamori waliwasukumiza wana wa Dani waende milimani; kwani hawakuwakubali kuteremkia bondeni;

Mpaka wa Waamori ulikuwa tangu huko kupandia Akrabimu, tangu hilo jabali, na juu yake.

Huyo Eloni, Mzabuloni, akafa, akazikwa katika Aiyaloni katika nchi ya Zabuloni.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo