Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 22:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

19 Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Mungu atamnyang'anya sehemu yake katika ule mti wa uhai, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyo vimeelezwa katika kitabu hiki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Kama mtu yeyote akipunguza humo chochote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule Mji Mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Kama mtu yeyote akipunguza humo chochote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:19
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na wafutwe katika kitabu cha uhai, Wala pamoja na wenye haki wasiandikwe.


BWANA akamwambia Musa, Mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye nitakayemfuta katika kitabu changu.


Usiongeze neno katika maneno yake; Asije akakulaumu, ukaonekana u mwongo.


Ole wenu, enyi wanasheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia, na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.


Neno lolote ninalowaagiza lizingatieni, usilizidishe, wala usilipunguze.


Msiliongeze neno ninalowaamuru wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, ninazowaamuru.


Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati uko karibu.


Na behewa lililo nje ya hekalu uliache nje wala usilipime, kwa maana Mataifa wamepewa hiyo, nao wataukanyaga mji mtakatifu miezi arubaini na miwili.


Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.


Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Na yeye ashindaye, na kuyatunza matendo yangu hata mwisho, nitampa mamlaka juu ya mataifa,


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.


Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe.


Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.


Tazama, naja upesi, na malipo yangu yako pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.


katikati ya njia yake kuu. Na upande huu na huu kando ya ule mto, ulikuwapo mti wa uzima, uzaao matunda, aina kumi na mbili, wenye kutoa matunda yake kila mwezi; na majani ya mti huo ni ya kuwaponya mataifa.


Na tazama, naja upesi; heri yeye ayashikaye maneno ya unabii wa kitabu hiki.


Yeye ashindaye, nitamfanya kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, wala hatatoka humo tena kabisa, nami nitaandika juu yake jina la Mungu wangu, na jina la mji wa Mungu wangu, huo Yerusalemu mpya, ushukao kutoka mbinguni kwa Mungu wangu, na jina langu mwenyewe, lile jipya.


Yeye ashindaye, nitamridhia kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo