Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 22:16 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

16 Mimi Yesu nimemtuma malaika wangu kuwashuhudia ninyi mambo hayo katika makanisa. Mimi ndimi niliye Shina na Mzawa wa Daudi, ile nyota yenye kung'aa ya asubuhi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 “Mimi, Yesu, nimemtuma malaika wangu awathibitishieni mambo haya katika makanisa. Mimi ni mzawa wa ukoo wa Daudi. Mimi ni nyota angavu ya asubuhi!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 “Mimi, Isa, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya jumuiya ya waumini. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi inayong’aa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 “Mimi, Isa, nimemtuma malaika wangu kushuhudia mambo haya kwa ajili ya jumuiya ya waumini. Mimi ndimi Shina na Mzao wa Daudi, ile Nyota ya Asubuhi ing’aayo.”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 22:16
30 Marejeleo ya Msalaba  

Basi litatoka chipukizi katika shina la Yese, na tawi litakalotoka katika mizizi yake litazaa matunda.


Jinsi ulivyoanguka kutoka mbinguni, Ewe nyota ya alfajiri, mwana wa asubuhi! Jinsi ulivyokatwa kabisa, Ewe uliyewaangusha mataifa!


ukamwambie, ukisema, BWANA wa majeshi asema hivi, ya kwamba, Tazama, mtu huyu ndiye ambaye jina lake ni Chipukizi; naye atakua katika mahali pake, naye atalijenga hekalu la BWANA.


Namwona, lakini si sasa; Namtazama, lakini si karibu; Nyota itatokea katika Yakobo Na fimbo ya enzi itainuka katika Israeli; Nayo itazipigapiga pembe za Moabu, Na kuwavunjavunja wana wote wa ghasia.


Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daudi, mwana wa Abrahamu.


Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia.


Ni mwana wa nani? Wakamwambia, Ni wa Daudi.


Basi, Daudi akimwita Bwana, amekuwaje ni mwanawe?


Kwa njia ya rehema za Mungu wetu, Ambazo kwa hizo mwangaza utokao juu umetufikia,


Basi Daudi amwita Bwana; amekuwaje mwana wake?


Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.


ambao mababu ni wao, na katika hao alitoka Kristo kwa jinsi ya mwili. Ndiye aliye juu ya mambo yote, Mungu, mwenye kuhimidiwa milele. Amina.


Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa iangazayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.


Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaoneshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonesha mtumwa wake Yohana;


ikisema, Haya uyaonayo uyaandike katika kitabu, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia.


Yohana, kwa yale makanisa saba yaliyoko Asia; Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwake yeye aliyeko na aliyekuwako na atakayekuja; na zitokazo kwa roho saba walioko mbele ya kiti chake cha enzi;


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.


Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo,


Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa.


Yeye ayashuhudiaye haya asema, Naam; naja upesi. Amina; na uje, Bwana Yesu.


Kisha akaniambia, Maneno haya ni amini na kweli. Naye Bwana, Mungu wa roho za manabii, alimtuma malaika wake kuwaonesha watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.


Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa.


Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo