Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 17:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

15 Kisha akaniambia, Yale maji uliyoyaona, hapo aketipo yule kahaba, ni jamaa na makutano na mataifa na lugha.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Malaika akaniambia pia, “Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi: Ni makundi ya watu wa kila taifa, rangi na lugha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Malaika akaniambia pia, “Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi: Ni makundi ya watu wa kila taifa, rangi na lugha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Malaika akaniambia pia, “Yale maji uliyoyaona pale alipokaa yule mzinzi: ni makundi ya watu wa kila taifa, rangi na lugha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Kisha yule malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa, makundi ya watu, mataifa na lugha.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Kisha yule malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona yule kahaba akiwa ameketi juu yake ni jamaa, makutano, mataifa na lugha.

Tazama sura Nakili




Ufunuo 17:15
14 Marejeleo ya Msalaba  

Kamba za mauti zilinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu.


Watuliza kuvuma kwa bahari, Kuvuma kwa mawimbi yake, Na ghasia za watu;


BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.


Ewe ukaaye juu ya maji mengi, uliye na hazina nyingi, mwisho wako umewadia, kadiri ya tamaa zako.


Bahari imefika juu ya Babeli, Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.


Maana BWANA amwangamiza Babeli, Na kuikomesha sauti kuu ndani yake; Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi, Mshindo wa sauti zao wafanya makelele;


Maji yalimlisha, vilindi vilimsitawisha; mito yake ilipita pande zote za miche yake; naye akatuma vijito vyake kwa miti yote ya shambani.


Wakaniambia, Imekupasa kutoa unabii tena juu ya watu na taifa na lugha na wafalme wengi.


Na watu wa hao jamaa na kabila na lugha na taifa waitazama mizoga yao siku tatu u nusu, wala hawaiachi mizoga yao kuwekwa kaburini.


Akaja mmoja wa wale malaika saba, wenye yale mabakuli saba, akanena nami, akisema, Njoo huku, nitakuonesha hukumu ya yule kahaba mkuu aketiye juu ya maji mengi;


Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo