Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Ufunuo 16:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Na huyo wa saba akalimimina bakuli lake juu ya anga. Sauti kuu ikatoka katika hekalu, katika kile kiti cha enzi, ikisema, Imekwisha kuwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Kisha, malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, hekaluni, ikisema, “Imetendeka!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Kisha, malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, hekaluni, ikisema, “Imetendeka!”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Kisha, malaika wa saba akamwaga bakuli lake hewani. Sauti kubwa ikasikika kutoka kwenye kiti cha enzi, hekaluni, ikisema, “Imetendeka!”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle Hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Malaika wa saba akamimina bakuli lake angani na sauti kubwa ikatoka mle hekaluni katika kile kiti cha enzi, ikisema, “Imekwisha kuwa!”

Tazama sura Nakili




Ufunuo 16:17
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.


ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;


Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.


Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.


Kisha hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la Agano lake likaonekana ndani ya hekalu lake. Kukawa na umeme, na sauti, na radi, na tetemeko la nchi, na mvua kubwa ya mawe.


Na malaika mwingine akatoka katika hekalu, akimlilia kwa sauti kuu yeye aliyekuwa ameketi juu ya lile wingu, Tia mundu wako, ukavune; kwa kuwa saa ya kuvuna imekuja; kwa kuwa mavuno ya nchi yamekomaa.


Kisha malaika mwingine akatoka katika lile hekalu lililoko mbinguni, yeye naye ana mundu mkali.


Nikasikia sauti kuu kutoka hekaluni, ikiwaambia wale malaika saba, Nendeni mkayamwage yale mabakuli saba ya ghadhabu ya Mungu juu ya nchi.


Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo