Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kitabu hiki si kilichoandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na si sehemu ya kanoni ya Kikristo wala Tanaki ya Kiyahudi. Kinaonyeshwa kwa madhumuni ya kihistoria na ya utafiti tu. Tazama maelezo kamili

Tobiti 6:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Basi yule jini ataisikia harufu yake na kukimbia, wala hatakuja tena kamwe. Lakini utakapomkaribia mkeo, ondokeni wote wawili na kumlilia Mungu mwenye rehema. Naye atawaokoa na kuwarehemuni. Nawe usiogope, kwa sababu umewekewa huyu tangu mwanzo. Nawe utamwokoa, naye atafuatana nawe; tena naona ya kuwa atakuzalia watoto. Basi alipoyasikia hayo, Tobia alimpenda, hata na roho yake ikaambatana naye kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Lakini kabla hamjalala pamoja, lazima msimame na kumwomba Mungu mwenye huruma awaokoe na kuwaoneeni huruma. Usiogope. Tangu mwanzo wa ulimwengu Sara alikuwa ameteuliwa awe mke wako. Utamwokoa kinywani mwa jini, naye atafuatana nawe mpaka nyumbani kwako. Wewe na Sara mtapata watoto wengi ambao mtawapenda sana. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi!” Basi, Tobia aliposikia maneno ya Rafaeli na kutambua kuwa Sara alikuwa jamaa yake kwa upande wa baba, alianza kumpenda Sara na kutamani sana kumwoa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Lakini kabla hamjalala pamoja, lazima msimame na kumwomba Mungu mwenye huruma awaokoe na kuwaoneeni huruma. Usiogope. Tangu mwanzo wa ulimwengu Sara alikuwa ameteuliwa awe mke wako. Utamwokoa kinywani mwa jini, naye atafuatana nawe mpaka nyumbani kwako. Wewe na Sara mtapata watoto wengi ambao mtawapenda sana. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi!”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Basi yule jini ataisikia harufu yake na kukimbia, wala hatakuja tena kamwe. Lakini utakapomkaribia mkeo, ondokeni wote wawili na kumlilia Mungu mwenye rehema. Naye atawaokoa na kuwarehemuni. Nawe usiogope, kwa sababu umewekewa huyu tangu mwanzo. Nawe utamwokoa, naye atafuatana nawe; tena naona ya kuwa atakuzalia watoto. Basi alipoyasikia hayo, Tobia alimpenda, hata na roho yake ikaambatana naye kabisa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

18 Lakini kabla hamjalala pamoja, lazima msimame na kumwomba Mungu mwenye huruma awaokoe na kuwaoneeni huruma. Usiogope. Tangu mwanzo wa ulimwengu Sara alikuwa ameteuliwa awe mke wako. Utamwokoa kinywani mwa jini, naye atafuatana nawe mpaka nyumbani kwako. Wewe na Sara mtapata watoto wengi ambao mtawapenda sana. Kwa hiyo usiwe na wasiwasi!” Basi, Tobia aliposikia maneno ya Rafaeli na kutambua kuwa Sara alikuwa jamaa yake kwa upande wa baba, alianza kumpenda Sara na kutamani sana kumwoa.

Tazama sura Nakili

Tobiti 6:18
0 Marejeleo ya Msalaba  

Tufuate:

Matangazo

Matangazo