Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Kitabu hiki si kilichoandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na si sehemu ya kanoni ya Kikristo wala Tanaki ya Kiyahudi. Kinaonyeshwa kwa madhumuni ya kihistoria na ya utafiti tu. Tazama maelezo kamili

Tobiti 10:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Akamwambia, Nyamaza wewe, usinidanganye, mwanangu amekufa. Naye hutoka kila siku kwenda katika njia waliyoiendea; wala hakula chakula mchana kutwa: wala hakukoma usiku kucha kumwombolezea mwanawe Tobia; hata zilipotimia zile siku kumi na nne za karamu ya arusi, ambazo Ragueli amemwapia akae huko siku hizo. Ndipo Tobia alipomwambia Ragueli, Niruhusu niende, maana baba yangu na mama yangu wanakata tamaa ya kuniona tena.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Lakini Ana akamjibu, “Niache usijaribu kunidanganya! Mwanangu amekufa!” Ikawa kila siku Ana alikuwa akitoka haraka nyumbani na kushinda kwenye barabara aliyoichukua Tobia wakati alipoanza safari yake, maana hakumwamini mtu mwingine. Jua lilipotua alirudi nyumbani akaomboleza na kulia usiku kucha bila kupata usingizi. Basi, yale majuma mawili ya sherehe ambayo Ragueli alikuwa ameapa kumfanyia binti yake yakaisha. Kwa hiyo Tobia akamwendea Ragueli akamwambia, “Tafadhali, uniache nirudi nyumbani, maana najua kwamba wazazi wangu hawana tena matumaini ya kuniona tena. Basi, nakuomba baba uniache niende nyumbani kwa baba yangu. Nimekwisha kukueleza hali niliyomwacha nayo nilipoondoka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

BIBLIA KISWAHILI

7 Akamwambia, Nyamaza wewe, usinidanganye, mwanangu amekufa. Naye hutoka kila siku kwenda katika njia waliyoiendea; wala hakula chakula mchana kutwa: wala hakukoma usiku kucha kumwombolezea mwanawe Tobia; hata zilipotimia zile siku kumi na nne za karamu ya harusi, ambazo Ragueli amemwapia akae huko siku hizo. Ndipo Tobia alipomwambia Ragueli, Niruhusu niende, maana baba yangu na mama yangu wanakata tamaa ya kuniona tena.

Tazama sura Nakili

BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA

7 Lakini Ana akamjibu, “Niache usijaribu kunidanganya! Mwanangu amekufa!” Ikawa kila siku Ana alikuwa akitoka haraka nyumbani na kushinda kwenye barabara aliyoichukua Tobia wakati alipoanza safari yake, maana hakumwamini mtu mwingine. Jua lilipotua alirudi nyumbani akaomboleza na kulia usiku kucha bila kupata usingizi. Basi, yale majuma mawili ya sherehe ambayo Ragueli alikuwa ameapa kumfanyia binti yake yakaisha. Kwa hiyo Tobia akamwendea Ragueli akamwambia, “Tafadhali, uniache nirudi nyumbani, maana najua kwamba wazazi wangu hawana tena matumaini ya kuniona tena. Basi, nakuomba baba uniache niende nyumbani kwa baba yangu. Nimekwisha kukueleza hali niliyomwacha nayo nilipoondoka.”

Tazama sura Nakili

Tobiti 10:7
0 Marejeleo ya Msalaba  

Tufuate:

Matangazo

Matangazo