Kitabu hiki si kilichoandikwa kwa uvuvio wa Mungu, na si sehemu ya kanoni ya Kikristo wala Tanaki ya Kiyahudi. Kinaonyeshwa kwa madhumuni ya kihistoria na ya utafiti tu. Tazama maelezo kamili Tobiti 10:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC12 Akamwambia binti yake, Waheshimu wakwezo, walio sasa kama wazazi wako; ili nipate sifa zako njema. Akambusu. Edna naye akamwambia Tobia, Ndugu yangu mpenzi, Mungu wa mbinguni akurudishe, na anijalie kuwaona watoto wako atakaokuzalia binti yangu Sara, ili nifurahi mbele za BWANA. Angalia, nimekukabidhi binti yangu amana bora, maana usimchokoze. Tazama suraBiblia Habari Njema - BHND12 Kisha akambusu binti yake Sara na kusema, “Nenda sasa nyumbani kwa baba mkwe wako, kwani tangu sasa wazazi wa mumeo ni wazazi wako kama sisi tulivyo wazazi wako. Nenda kwa amani, binti yangu. Natumaini kusikia mema juu yako kadiri niishivyo.” Kisha akawaaga na kuwaacha waende zao. Naye Edna akamwambia Tobia, “Mwanangu mpendwa na ndugu Tobia, Bwana wa mbinguni akurudishe tena salama! Nami natumaini kuishi hata niwaone watoto wako na binti yangu Sara kabla sijafa. Mbele ya Bwana namkabidhi binti yangu mikononi mwako. Kamwe usimhuzunishe maishani mwako. Nenda kwa amani mwanangu. Tangu sasa mimi ni mama yako na Sara ni dada yako mpendwa. Na sote tuishi kwa amani siku zote za maisha yetu!” Basi akawabusu wote wawili na kuwaacha kwa furaha. Tazama suraBiblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza12 Kisha akambusu binti yake Sara na kusema, “Nenda sasa nyumbani kwa baba mkwe wako, kwani tangu sasa wazazi wa mumeo ni wazazi wako kama sisi tulivyo wazazi wako. Nenda kwa amani, binti yangu. Natumaini kusikia mema juu yako kadiri niishivyo.” Kisha akawaaga na kuwaacha waende zao. Naye Edna akamwambia Tobia, “Mwanangu mpendwa na ndugu Tobia, Bwana wa mbinguni akurudishe tena salama! Nami natumaini kuishi hata niwaone watoto wako na binti yangu Sara kabla sijafa. Mbele ya Bwana namkabidhi binti yangu mikononi mwako. Kamwe usimhuzunishe maishani mwako. Nenda kwa amani mwanangu. Tangu sasa mimi ni mama yako na Sara ni dada yako mpendwa. Na sote tuishi kwa amani siku zote za maisha yetu!” Basi akawabusu wote wawili na kuwaacha kwa furaha. Tazama suraBIBLIA KISWAHILI12 Akamwambia binti yake, Waheshimu wakwezo, walio sasa kama wazazi wako; ili nipate sifa zako njema. Akambusu. Edna naye akamwambia Tobia, Ndugu yangu mpenzi, Mungu wa mbinguni akurudishe, na anijalie kuwaona watoto wako atakaokuzalia binti yangu Sara, ili nifurahi mbele za BWANA. Angalia, nimekukabidhi binti yangu amana bora, kwa hiyo usimchokoze. Tazama suraBIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA12 Kisha akambusu binti yake Sara na kusema, “Nenda sasa nyumbani kwa baba mkwe wako, kwani tangu sasa wazazi wa mumeo ni wazazi wako kama sisi tulivyo wazazi wako. Nenda kwa amani, binti yangu. Natumaini kusikia mema juu yako kadiri niishivyo.” Kisha akawaaga na kuwaacha waende zao. Naye Edna akamwambia Tobia, “Mwanangu mpendwa na ndugu Tobia, Bwana wa mbinguni akurudishe tena salama! Nami natumaini kuishi hata niwaone watoto wako na binti yangu Sara kabla sijafa. Mbele ya Bwana namkabidhi binti yangu mikononi mwako. Kamwe usimhuzunishe maishani mwako. Nenda kwa amani mwanangu. Tangu sasa mimi ni mama yako na Sara ni dada yako mpendwa. Na sote tuishi kwa amani siku zote za maisha yetu!” Basi akawabusu wote wawili na kuwaacha kwa furaha. Tazama sura |