Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Sefania 3:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

12 Lakini nitabakiza ndani yako watu walioonewa na maskini, nao watalitumainia jina la BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Nitakuachia watu wapole na wanyenyekevu ambao watakimbilia usalama kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Nitakuachia watu wapole na wanyenyekevu ambao watakimbilia usalama kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Nitakuachia watu wapole na wanyenyekevu ambao watakimbilia usalama kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Lakini nitakuachia ndani yako wapole na wanyenyekevu, ambao wanatumaini jina la Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Lakini nitakuachia ndani yako wapole na wanyenyekevu, ambao wanatumaini jina la bwana.

Tazama sura Nakili




Sefania 3:12
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na BWANA, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu.


Naye BWANA huwasaidia na kuwaopoa; Huwaopoa kutoka kwa wasio haki na kuwaponya; Kwa kuwa wamemtumaini Yeye.


Nao walio maskini kabisa watakula, Na wahitaji watajilaza salama; Nami nitatia shina lako kwa njaa, Na mabaki yako watauawa.


Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.


Wanyenyekevu nao wataongeza furaha yao katika BWANA, na maskini katika wanadamu watafurahi katika Mtakatifu wa Israeli.


Ni nani miongoni mwenu amchaye BWANA, aitiiye sauti ya mtumishi wake? Yeye aendaye katika giza, wala hana nuru, naye alitumainia jina la BWANA, na kumtegemea Mungu wake.


Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.


Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini lake.


Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa Israeli utatafutwa, wala hakuna uovu; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.


Lakini nitasaza mabaki; maana mtakuwa na baadhi ya watu watakaoukimbia upanga kati ya mataifa, mtakapokuwa mmetawanyika katika nchi za watu.


Nao wataiharibu nchi ya Ashuru kwa upanga, na nchi ya Nimrodi katika malango yake; naye atatuokoa na Mwashuri, atakapoingia katika nchi yetu, na kukanyaga ndani ya mipaka yetu.


BWANA ni mwema, ni ngome siku ya taabu; naye huwajua hao wamkimbiliao.


Nayo ikavunjwa siku ile; na hivyo wale kondoo wanyonge walionisikiliza wakajua ya kuwa neno hili ndilo neno la BWANA.


Basi nikalilisha kundi la machinjo, kweli kondoo waliokuwa wanyonge kabisa. Kisha nikajipatia fimbo mbili; nami nikaiita ya kwanza, Neema, na ya pili nikaiita, Umoja; nikalilisha kundi lile.


vipofu wanapata kuona, viwete wanakwenda, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanahubiriwa Habari Njema.


Na jina lake Mataifa watalitumainia.


Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.


Na tena Isaya anena, Litakuwako shina la Yese, Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa; Ndiye Mataifa watakayemtumaini.


Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


na kupitia kwake mmekuwa wenye kumwamini Mungu, aliyemfufua katika wafu akampa utukufu; hata imani yenu na tumaini lenu liwe kwa Mungu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo