Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Sefania 2:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

9 Basi kama niishivyo, asema BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, Hakika Moabu atakuwa kama Sodoma, na wana wa Amoni kama Gomora, yaani, milki ya upupu, na mashimo ya chumvi, ukiwa wa daima; watu wangu waliosalia watawateka nyara, na watu wa taifa langu waliobaki watawarithi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Kwa hiyo, niishivyo mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, mimi Mungu wa Israeli, Moabu itakuwa kama Sodoma na Amoni itakuwa kama Gomora. Nchi zake zitakuwa za viwavi na mashimo ya chumvi, zitakuwa ukiwa milele. Watu wangu watakaobaki wataziteka nyara, watu wa taifa langu waliosalia watazimiliki.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Hakika, kama niishivyo,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamoni kama Gomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Hakika, kama niishivyo,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote, Mungu wa Israeli, “hakika Moabu itakuwa kama Sodoma, Waamoni kama Gomora: mahali pa magugu na mashimo ya chumvi, nchi ya ukiwa milele. Mabaki ya watu wangu watawateka nyara; mabaki ya taifa langu watarithi nchi yao.”

Tazama sura Nakili




Sefania 2:9
27 Marejeleo ya Msalaba  

Nao watashuka, watalirukia bega la Wafilisti upande wa magharibi; nao pamoja watawateka wana wa mashariki; watanyosha mkono juu ya Edomu na Moabu; na wana wa Amoni watawatii.


Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji machafu.


Inua macho yako, ukatazame pande zote; hao wote wanajikusanya na kukujia. Kama niishivyo, asema BWANA, hakika utajivika hao wote kama pambo, nawe utajipamba kwao kama bibi arusi.


Kama mimi niishivyo, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi, hakika yake, kama Tabori katika milima, na kama Karmeli karibu na bahari, ndivyo atakavyokuja.


Kuhusu Moabu. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.


Kuhusu wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake?


Kama vile vilivyotokea wakati wa kuangushwa Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; hapana mtu atakayekaa huko, wala hapana mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.


Na Hazori utakuwa kao la mbwamwitu; ukiwa milele; hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama mgeni akaavyo.


Kama vile ilivyotokea Mungu alipoangusha Sodoma na Gomora, na miji iliyokuwa karibu nayo, asema BWANA; kadhalika hakuna mtu atakayekaa huko, wala hakuna mwanadamu atakayekaa huko kama wageni wakaavyo.


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa; Sef 2:8-11; 2 Fal 3:27


Na makundi ya wanyama watalala kati yake, wanyama wote wa mataifa; bundi na kunguru watakaa juu ya vichwa vya nguzo zake; sauti yao itasikiwa madirishani; vizingitini mwake mtakuwa ukiwa; kwa maana ameifunua kazi ya mierezi.


Na hiyo nchi ya pwani itakuwa nchi ya watu wa nyumba ya Yuda waliosalia; watachunga makundi yao huko; watalala katika nyumba za Ashkeloni wakati wa jioni; kwa maana BWANA, Mungu wao, atawajia na kuwarudisha wafungwa wao.


Mabaki ya Israeli hawatatenda uovu, wala kusema uongo; wala ulimi wa hadaa hautakuwa kinywani mwao; kwa maana watakula na kulala, wala hapana mtu atakayewatisha.


Nyamazeni, ninyi nyote wenye mwili, mbele za BWANA; kwa maana ameamka, na kutoka katika maskani yake takatifu.


lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;


Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.


Na kizazi cha baadaye, wanenu watakaoinuka baada yenu, na mgeni atakayekuja kutoka nchi ya mbali, watasema, watakapoyaona mapigo ya nchi ile, na magonjwa aliyoitia BWANA;


ya kuwa nchi yake nzima ni kibiriti, na chumvi, na kuteketea, haipandwi, wala haizai, wala nyasi hazimei humo, kama mapinduko ya Sodoma na Gomora, Adma na Seboimu, aliyoipindua BWANA kwa ghadhabu yake na hasira zake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo