Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Sefania 2:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

8 Mimi nimeyasikia masuto ya Moabu, na dhihaka za wana wa Amoni, ambazo kwa hizo wamewatukana watu wangu, na kujitukuza juu ya mpaka wao. 21:28-32; 25:1-11; Amo 1:13-15

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Nimeyasikia masuto ya Moabu na dhihaka za Waamoni; jinsi walivyowasuta watu wangu, na kujigamba kuiteka nchi yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Nimeyasikia masuto ya Moabu na dhihaka za Waamoni; jinsi walivyowasuta watu wangu, na kujigamba kuiteka nchi yao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Nimeyasikia masuto ya Moabu na dhihaka za Waamoni; jinsi walivyowasuta watu wangu, na kujigamba kuiteka nchi yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 “Nimeyasikia matukano ya Moabu nazo dhihaka za Waamoni, ambao waliwatukana watu wangu na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 “Nimeyasikia matukano ya Moabu nazo dhihaka za Waamoni, ambao waliwatukana watu wangu na kutoa vitisho dhidi ya nchi yao.

Tazama sura Nakili




Sefania 2:8
19 Marejeleo ya Msalaba  

Yule mkubwa akazaa mwana, akamwita jina lake Moabu; huyo ndiye baba wa Wamoabi, hata leo.


Na yule mdogo naye akazaa mwana akamwita jina lake Benami; huyo ndiye baba wa Waamoni hata leo.


Ufunuo juu ya Moabu. Maana katika usiku mmoja Ari wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa; maana katika usiku mmoja Kiri wa Moabu umeharibiwa kabisa na kuangamizwa.


Tumesikia habari za kiburi cha Moabu, ya kwamba ni mwenye kiburi kingi; habari za majivuno yake, na kiburi chake, na ghadhabu yake; majivuno yake si kitu.


BWANA asema hivi juu ya jirani zangu wote walio wabaya, waugusao urithi wangu niliowarithisha watu wangu Israeli, Tazama, nitawang'oa katika nchi yao, nami nitaing'oa nyumba ya Yuda isiwe kati yao.


Kuhusu Moabu. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.


Kuhusu wana wa Amoni. BWANA asema hivi, Je, Israeli hana wana? Je! Hana mrithi? Basi, mbona Malkamu anamiliki Gadi, na watu wake wanakaa katika miji yake?


Ee BWANA, umeyasikia matukano yao, Na mashauri yao yote juu yangu;


Nawe, mwanadamu, tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu wana wa Amoni, na kuhusu aibu yao; Nena, Upanga; upanga umefutwa; umeng'arishwa, ili kuua, ili kuufanya uue sana, upate kuwa kama umeme;


Neno la BWANA likanijia, kusema,


Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matusi yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.


Bwana MUNGU asema hivi; Kwa sababu adui amesema juu yenu, Aha! Na, Mahali pa juu pa zamani pamekuwa petu tupamiliki;


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya wana wa Amoni, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu wamewapasua wanawake wa Gileadi wenye mimba, ili wapate kuongeza mipaka yao;


Haya ndiyo asemayo BWANA; Kwa makosa matatu ya Moabu, naam, kwa manne, sitaizuia adhabu yake isimpate; kwa sababu aliichoma moto mifupa ya mfalme wa Edomu hata ikawa chokaa; Sef 2:8-11; 2 Fal 3:27


Mambo hayo yatawapata kwa sababu ya kiburi chao, kwa kuwa wamewatukana watu wa BWANA wa majeshi, na kujitukuza juu yao.


BWANA akamwambia Yoshua, Siku hii ya leo nimeivingirisha hiyo aibu ya Misri iondoke juu yenu. Kwa hiyo jina la mahali pale likaitwa Gilgali, hata hivi leo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo