Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Ruthu 3:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

7 Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa rundo la nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alienda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala.

Tazama sura Nakili




Ruthu 3:7
18 Marejeleo ya Msalaba  

Wakapelekewa sehemu za chakula kutoka mezani pake, lakini akazidisha sehemu ya Benyamini iwe kubwa mara tano kuliko zao. Wakanywa, wakafurahi pamoja naye.


Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, kisha mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, na wenye ujasiri.


Yezebeli mkewe akamwambia, Je! Sasa wewe unaumiliki ufalme wa Israeli? Ondoka, ule chakula, moyo wako ufurahi; mimi nitakupa shamba la mizabibu la Nabothi Myezreeli.


Katika siku ya saba, mfalme alipofurahiwa moyo wake kwa divai, aliwaamuru Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari, na Karkasi, wale Matowashi saba, wasimamizi wa nyumba saba waliohudumu mbele zake,


Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.


Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote.


Mwanadamu hapati jema kupita kula na kunywa, na kuiburudisha roho yake kwa mema katika kazi yake. Hayo nayo niliona ya kwamba hutoka mkononi mwa Mungu.


Kisha nikaisifu furaha, kwa sababu mwanadamu hana neno lolote lililo jema chini ya jua, kuliko kula, kunywa, na kujifurahisha; maana hili atakaa nalo katika amali yake, siku zote za maisha yake alizompa Mungu chini ya jua.


Wewe nenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.


Basi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.


Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;


Ikawa mioyo yao iliposhangilia, wakasema, Mwiteni Samsoni, ili atufanyie michezo. Basi wakamwita Samsoni atoke gerezani, akacheze mbele yao wakamweka katikati ya nguzo mbili.


Hapo walipokuwa wakifurahisha mioyo yao, tazama, watu wa mji huo, watu mabaradhuli wakaizingira hiyo nyumba pande zote, wakagonga mlango; wakasema na huyo mwenye nyumba, huyo mzee, na kumwambia, Mlete nje mtu yule aliyefika nyumbani kwako, ili tupate kumjua.


Basi wakaketi, wakala na kunywa wote wawili pamoja; kisha baba yake mwanamke akamwambia huyo mtu, Uwe radhi, tafadhali, ukae usiku kucha, na moyo wako na ufurahi.


Kisha hapo mtu huyo alipoinuka ili aende zake, yeye na suria wake, na mtumishi wake, huyo mkwewe, baba yake mwanamke, akamwambia, Tazama mchana wakaribia jioni, tafadhali kaa usiku kucha; tazama mchana wakaribia mwisho wake, lala hapa, ili moyo wako ufurahi; hata kesho uende zako asubuhi na mapema, ili upate kwenda kwenu.


Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza.


Na ikawa usiku wa manane yule mtu akashtuka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo