Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Obadia 1:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

20 Na watu wa jeshi hili la wana wa Israeli waliotekwa, walio kati ya Wakanaani, watamiliki mpaka Sarepta; na hao watu wa Yerusalemu waliotekwa, waliomo Sefaradi, wataimiliki miji ya Negebu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Waisraeli walio uhamishoni Hala wataimiliki Foinike hadi Sarepta. Watu wa Yerusalemu walio uhamishoni Sefaradi wataimiliki miji ya Negebu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Waisraeli walio uhamishoni Hala wataimiliki Foinike hadi Sarepta. Watu wa Yerusalemu walio uhamishoni Sefaradi wataimiliki miji ya Negebu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Waisraeli walio uhamishoni Hala wataimiliki Foinike hadi Sarepta. Watu wa Yerusalemu walio uhamishoni Sefaradi wataimiliki miji ya Negebu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kundi la Waisraeli walio uhamishoni Kanaani watarudi na kuimiliki nchi hadi Sarepta. Walio uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu wataimiliki miji ya Negebu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kundi la Waisraeli walioko uhamishoni Kanaani watarudi na kumiliki nchi mpaka Sarepta. Walioko uhamishoni Sefaradi kutoka Yerusalemu watamiliki miji ya Negebu.

Tazama sura Nakili




Obadia 1:20
12 Marejeleo ya Msalaba  

Miji ya Negebu imefungwa malango yake, wala hapana mtu wa kuyafungua; Yuda amechukuliwa mateka; amechukuliwa kabisa mateka.


Siku zile nyumba ya Yuda watakwenda pamoja na nyumba ya Israeli, nao watakuja pamoja, kutoka nchi ya kaskazini, mpaka nchi ile niliyowapa baba zenu iwe urithi wao.


Watu watanunua mashamba kwa fedha, watazitia sahihi hati zake, na kuzipiga mhuri, na kuwaita mashahidi, katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo pande zote za Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, na katika miji ya nchi yenye vilima, na katika miji ya nchi tambarare, na katika miji ya Negebu; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, asema BWANA.


Katika miji ya nchi ya vilima, katika miji ya nchi tambarare, katika miji ya Negebu, na katika nchi ya Benyamini, na katika mahali palipo karibu na Yerusalemu, na katika miji ya Yuda, makundi ya kondoo yatapita tena chini ya mikono yake anayewahesabu, asema BWANA.


ndipo nitawatupilia mbali wazao wa Yakobo, na Daudi, mtumishi wangu, hata nisitwae wazao wake watawale juu ya wazao wa Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa maana nitawarudisha wafungwa wao, nami nitawarehemu.


Naam, nitaleta watu watembee juu yenu, naam, watu wangu Israeli; nao watakumiliki, nawe utakuwa urithi wao, wala hutawaua watoto wao tena tangu leo.


wala Eliya hakutumwa kwa mmojawapo, ila kwa mjane mmoja wa Sarepta katika nchi ya Sidoni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo