Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Nahumu 3:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

17 Watu wako waliotiwa taji ni kama nzige, na majemadari wako ni kama makundi ya mapanzi, watuao katika vitalu siku ya baridi, lakini jua lipandapo huruka juu na kwenda zao, wala hapana ajuaye walikokwenda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

17 Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

17 Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

17 Wakuu wako ni kama panzi, maofisa wako kama kundi la nzige; wakati wa baridi wanakaa kwenye kuta, lakini jua lichomozapo, huruka, wala hakuna ajuaye walikokwenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

17 Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako kama makundi ya nzige wanaotua kwenye kuta wakati wa siku ya baridi; lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna anayejua wanakoenda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

17 Walinzi wako ni kama nzige, maafisa wako ni kama makundi ya nzige watuao kwenye kuta wakati wa siku ya baridi: lakini wakati jua linapotokea wanaruka kwenda zao, na hakuna ajuaye waendako.

Tazama sura Nakili




Nahumu 3:17
4 Marejeleo ya Msalaba  

Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu.


Na wageni, watu wa mataifa watishao, wamemkatilia mbali na kumwacha; juu ya milima na katika mabonde yote matawi yake yameanguka, na vitanzu vyake vimevunjika karibu na mifereji yote ya nchi; na watu wote wa dunia wameshuka, wakitoka katika uvuli wake na kumwacha.


Chukueni nyara za fedha; Chukueni nyara za dhahabu; Kwa maana ni akiba isiyoisha, Fahari ya vyombo vipendezavyo.


Na maumbo ya hao nzige yalikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita, na juu ya vichwa vyao kama mataji, mfano wa dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama nyuso za wanadamu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo