Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mwanzo 44:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Wakararua nguo zao, wakaweka kila mtu mzigo wake juu ya punda wake, wakarudi mjini.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Hapo wakayararua mavazi yao kwa huzuni. Kila mmoja wao akambebesha punda wake mzigo wake, wakarudi mjini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Hapo wakayararua mavazi yao kwa huzuni. Kila mmoja wao akambebesha punda wake mzigo wake, wakarudi mjini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Hapo wakayararua mavazi yao kwa huzuni. Kila mmoja wao akambebesha punda wake mzigo wake, wakarudi mjini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Kwa hilo, wakararua nguo zao. Ndipo wote wakapakiza mizigo yao juu ya punda wao na kurudi mjini.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Kwa jambo hili, wakararua nguo zao. Ndipo wote wakapakiza mizigo yao juu ya punda zao na kurudi mjini.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 44:13
7 Marejeleo ya Msalaba  

Na walipotoka mjini, kabla hawajaendelea sana, Yusufu akamwambia yule msimamizi wa nyumba yake, Ondoka, uwafuate watu hawa, nawe utakapowapata, waambie, Kwa nini mmelipa mabaya kwa mema?


Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye;


hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.


Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti.


akatazama, na tazama, mfalme amesimama karibu na nguzo kama ilivyokuwa desturi, nao wakuu na wapiga baragumu karibu na mfalme; na watu wote wa nchi wakafurahi, wakapiga baragumu. Ndipo Athalia akararua mavazi yake, akalia, Uhaini! Uhaini!


Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo