Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 43:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

28 Wakasema, Mtumishi wako baba yetu hajambo, angali hai; wakainama, wakasujudu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

28 Wakamjibu, “Mtumishi wako, baba yetu, hajambo na angali hai.” Kisha wakainama kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

28 Wakamjibu, “Mtumishi wako, baba yetu, hajambo na angali hai.” Kisha wakainama kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

28 Wakamjibu, “Mtumishi wako, baba yetu, hajambo na angali hai.” Kisha wakainama kwa heshima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

28 Wakamjibu, “Mtumishi wako, baba yetu, bado anaishi na ni mzima.” Kisha wakainama, wakamsujudia.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

28 Wakamjibu, “Mtumishi wako baba yetu bado anaishi na ni mzima.” Kisha wakainama chini kumpa heshima.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 43:28
8 Marejeleo ya Msalaba  

Tazama, sisi tulikuwa tukifunga miganda shambani, kumbe! Mganda wangu ukaondoka ukasimama, na tazama, miganda yenu ikazunguka ikainama mbele ya mganda wangu.


Alipokuja Yusufu nyumbani, wakamletea ile zawadi iliyokuwa mikononi mwao nyumbani mwake, wakamwinamia mpaka chini.


hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.


Naye yule mwanamke wa Tekoa aliponena na mfalme, akaanguka kifudifudi chini, akamsujudia, akasema, Nisaidie, Ee mfalme.


Bathsheba akainama, akamsujudia mfalme. Naye mfalme akamwuliza, Wataka nini?


Hata baada ya kufa kwake Yehoyada, wakuu wa Yuda wakamwendea mfalme, wakamsujudia. Naye mfalme akawasikiliza maneno yao.


Basi Musa akatoka nje ili amlaki mkwewe, akasujudia na kumbusu; nao wakaulizana habari; kisha wakaingia hemani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo