Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mwanzo 38:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

14 Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 alivua mavazi yake ya ujane na kujifunika shela kisha akaketi penye lango la kuingilia Enaimu, kijiji kilichokuwa njiani kwenda Timna. Alifanya hivyo kwa vile aliona kwamba Shela alikwisha kuwa mtu mzima, lakini yeye Tamari hakuozwa awe mkewe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 alivua mavazi yake ya ujane na kujifunika shela kisha akaketi penye lango la kuingilia Enaimu, kijiji kilichokuwa njiani kwenda Timna. Alifanya hivyo kwa vile aliona kwamba Shela alikwisha kuwa mtu mzima, lakini yeye Tamari hakuozwa awe mkewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike. Akaketi kwenye mlango wa Enaimu, njiani ya kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba ingawa Shela sasa alikuwa mtu mzima, bado hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 alivua mavazi yake ya ujane, akajifunika kwa shela ili asifahamike, akaketi kwenye mlango wa Enaimu, ambao upo njiani kuelekea Timna. Akafanya hivyo kwa sababu aliona kwamba, ingawa Shela amekua, lakini alikuwa hajakabidhiwa kwake kuwa mkewe.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 38:14
9 Marejeleo ya Msalaba  

Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye shambani kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika.

Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba, maana amejifunika uso.

Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake.

Yuda akavikiri, akasema, Yeye ni mwenye haki kuliko mimi, kwa kuwa sikumpa Shela, mwanangu. Wala hakumjua tena baada ya hayo.

Na tazama, mwanamke akamkuta, Ana mavazi ya kikahaba, mwerevu wa moyo;

Mara yuko katika njia kuu, mara viwanjani, Naye huotea kwenye pembe za kila njia.

Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pako wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.

Umejenga mahali pako palipoinuka penye kichwa cha kila njia, ukaufanya uzuri wako kuwa chukizo, ukatanua miguu yako kwa kila mtu aliyepita karibu, ukaongeza mambo yako ya kikahaba.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo