Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 37:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

18 Wakamwona akiwa mbali, na kabla hajawakaribia, wakafanya shauri juu yake ili wamwue.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali na kabla hajafika karibu, wakafanya mpango wa kumuua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali na kabla hajafika karibu, wakafanya mpango wa kumuua.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali na kabla hajafika karibu, wakafanya mpango wa kumuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga njama za kumuua.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Ndugu zake walipomwona akiwa mbali, kabla hajawafikia, wakapanga shauri baya la kumuua.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 37:18
19 Marejeleo ya Msalaba  

Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.


Wakasemezana wao kwa wao, Tazama, yule bwana wa ndoto anakuja.


Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda.


Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo.


Akawageuza moyo wawachukie watu wake, Wakawatendea hila watumishi wake.


Badala ya upendo wangu wao hunishitaki, Ijapokuwa niliwaombea.


Maana nimesikia wengi wakinong'onezana; Hofu katika pande zote. Waliposhauriana juu yangu, Walipanga kunitoa uhai wangu.


Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA, Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.


Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki, Na kumsagia meno yake.


Mtu asiye haki humvizia mwenye haki, Na kutafuta jinsi ya kumwua.


Kwa pamoja wanaishambulia nafsi yake mwenye haki, Na kuihukumu damu isiyo na hatia.


Lakini wale wakulima walipomwona yule mwana, wakasemezana wao kwa wao, Huyu ni mrithi; haya na tumwue, tuutwae urithi wake.


Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;


Lakini wale wakulima wakasemezana, Huyu ni mrithi; haya, na tumwue, na urithi utakuwa wetu.


Baada ya siku mbili ilikuwa sikukuu ya Pasaka, na mikate isiyochachwa; wakuu wa makuhani na waandishi wakatafuta njia ya kumkamata kwa hila na kumwua.


Basi tangu siku ile walifanya shauri la kumwua.


Kulipopambazuka, Wayahudi wakafanya mapatano, wakajifunga kwa kiapo kwamba hawatakula wala hawatakunywa hadi wamwue Paulo.


Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo