Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 35:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 akafariki akiwa mzee wa miaka mingi. Watoto wake, Esau na Yakobo wakamzika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 akafariki akiwa mzee wa miaka mingi. Watoto wake, Esau na Yakobo wakamzika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 akafariki akiwa mzee wa miaka mingi. Watoto wake, Esau na Yakobo wakamzika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Kisha Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho, akafa; akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee aliyeshiba siku. Nao Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Kisha Isaka akapumua pumzi yake ya mwisho akafa, akakusanywa pamoja na watu wake akiwa mzee wa miaka mingi. Nao wanawe Esau na Yakobo wakamzika.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 35:29
13 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.


Ishmaeli aliishi miaka mia moja na thelathini na saba. Akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake.


Esau akamchukia Yakobo kwa ajili ya ile baraka babaye aliyombariki. Esau akasema moyoni mwake, Siku za kumlilia baba yangu zinakaribia, ndipo nitakapomwua ndugu yangu Yakobo.


kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.


Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, akasema, La! Nitashuka kaburini kwa mwanangu, nikiomboleza. Basi baba yake akamlilia.


Lakini nitakapolala pamoja na baba zangu, unichukue toka Misri, unizike katika kaburi lao. Akasema, Nitafanya kama ulivyosema.


Humo walimzika Abrahamu, na Sara mkewe; humo wakamzika Isaka, na Rebeka mkewe; nami humo nikamzika Lea;


Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.


Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo