Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mwanzo 31:32 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

32 Awaye yote utakayemwona kuwa nayo miungu yako, yeye asiishi. Mbele ya ndugu zetu ukitambue kilicho chako kwangu, ukakichukue. Maana Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Lakini utakayempata na vinyago vya miungu yako asiishi! Mbele ya hawa ndugu zetu, onesha chochote kilicho chako, ukichukue.” Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba vinyago vya miungu ya Labani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Lakini utakayempata na vinyago vya miungu yako asiishi! Mbele ya hawa ndugu zetu, onesha chochote kilicho chako, ukichukue.” Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba vinyago vya miungu ya Labani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Lakini utakayempata na vinyago vya miungu yako asiishi! Mbele ya hawa ndugu zetu, onesha chochote kilicho chako, ukichukue.” Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba vinyago vya miungu ya Labani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Lakini ukimkuta yeyote na miungu yako, huyo mtu hataishi. Mbele ya jamaa zetu, angalia mwenyewe uone kama kuna chochote chako hapa nilicho nacho; kama kipo, kichukue.” Basi Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiiba hiyo miungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Lakini kama ukimkuta yeyote aliye na miungu yako, hataishi. Mbele ya jamaa yetu, angalia mwenyewe uone kama kuna chochote chako hapa nilicho nacho, kama kipo, kichukue.” Basi Yakobo hakujua kwamba Raheli alikuwa ameiba hiyo miungu.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 31:32
13 Marejeleo ya Msalaba  

Abramu akamwambia Lutu, Basi, usiwepo ugomvi, nakusihi, kati yangu na wewe, wala kati ya wachungaji wangu na wachungaji wako; maana sisi tu jamaa moja.


Akasema, Basi, nawasihi, ndugu zangu, msitende vibaya hivi.


Na haki yangu itanishuhudia katika siku zijazo, utakapokuja kwa habari ya mshahara wangu ulioko kwako. Kila asiye madoadoa au marakaraka katika mbuzi, au asiye mweusi katika kondoo, akionekana kwangu, itahesabiwa kuwa ameibiwa.


Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye.


akatwaa ndugu zake pamoja naye, akamfuata mwendo wa siku saba. Akampata katika mlima wa Gileadi.


Basi sasa, umetoka kwa sababu umetamani sana nyumba ya baba yako. Mbona basi umeiiba miungu yangu?


Yakobo akajibu, akamwambia Labani, Kwa sababu niliogopa, nikasema, Usije ukaninyang'anya binti zako kwa nguvu.


Labani akaingia katika hema ya Yakobo, na hema ya Lea, na hema ya vijakazi wawili, wala hakuiona. Akatoka katika hema ya Lea, akaingia katika hema ya Raheli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo