Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 28:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

13 Na tazama, BWANA amesimama juu yake, akasema, Mimi ni BWANA, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka; nchi hii unayolala nitakupa wewe na uzao wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

13 Mwenyezi-Mungu alisimama juu ya ngazi hiyo, akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi unayoilalia nitakupa wewe na wazawa wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

13 Mwenyezi-Mungu alisimama juu ya ngazi hiyo, akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi unayoilalia nitakupa wewe na wazawa wako.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

13 Mwenyezi-Mungu alisimama juu ya ngazi hiyo, akamwambia, “Mimi ndimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Abrahamu baba yako, na Mungu wa Isaka. Nchi unayoilalia nitakupa wewe na wazawa wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

13 Juu yake alisimama Mwenyezi Mungu, akasema, “Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba yako Ibrahimu, na Mungu wa Isaka. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

13 Juu yake alisimama bwana, akasema, “Mimi ni bwana, Mungu wa baba yako Ibrahimu na Mungu wa Isaka. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 28:13
40 Marejeleo ya Msalaba  

BWANA akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa nchi hii. Naye akamjengea BWANA madhabahu huko alikomtokea.


maana nchi hii yote uionayo, nitakupa wewe na uzao wako hata milele.


Ondoka, ukatembee katika nchi hii katika mapana yake, na marefu yake, maana nitakupa wewe nchi hiyo.


Baada ya mambo hayo neno la BWANA likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako itakuwa kubwa sana.


Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,


BWANA akamtokea usiku uleule, akasema, Mimi ni Mungu wa Abrahamu baba yako, usiogope, maana mimi ni pamoja nawe, nami nitakubariki, na kuzidisha uzao wako kwa ajili ya Abrahamu mtumishi wangu.


Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako.


Akupe baraka ya Abrahamu, wewe na uzao wako pamoja nawe, upate kuirithi nchi ya kusafiri kwako, Mungu aliyompa Abrahamu.


Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.


Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Abrahamu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.


Naona uso wa baba yenu, kwamba hanitazami vema kama hapo awali. Lakini Mungu wa baba yangu amekuwa pamoja nami.


Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.


mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.


Yakobo akasema, Ee Mungu wa baba yangu Abrahamu, na Mungu wa baba yangu Isaka, BWANA, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako, na kwa jamaa zako, nami nitakutendea mema;


Mungu akamwambia Yakobo, Ondoka, panda uende Betheli, ukakae huko; ukamfanyie Mungu madhabahu huko; yeye aliyekutokea ulipomkimbia Esau, ndugu yako.


Na nchi hii niliyowapa Abrahamu na Isaka nitakupa wewe, na uzao wako baada yako nitawapa nchi hiyo.


Yakobo akapaita mahali pale, Mungu aliposema naye, Betheli.


Ikawa alipokuwa anashikwa sana na uchungu, mkunga akamwambia, Usiogope, maana sasa utamzaa mwanamume mwingine.


Akasema, Mimi ni Mungu, Mungu wa baba yako, usiogope kushuka mpaka Misri; maana nitakufanya uwe taifa kubwa huko.


Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,


Agano alilofanya na Abrahamu, Na kiapo chake kwa Isaka;


Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Iwe urithi wenu mliopimiwa;


Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani, Kama fungu la urithi wenu.


Mungu akasikia kuugua kwao, Mungu akakumbuka agano lake alilolifanya na Abrahamu na Isaka na Yakobo.


Tena akasema, Mimi ni Mungu wa baba yako, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Musa akafunika uso wake; kwa maana aliogopa kumwangalia Mungu.


ili kwamba wapate kusadiki ya kwamba BWANA, Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, Mungu wa Yakobo, amekutokea.


Tena nimelithibitisha agano langu nao, la kuwapa nchi ya Kanaani; nchi ya waliyokaa kama wageni.


nami nitawatwaeni kuwa watu wangu, nitakuwa Mungu kwenu; nanyi mtajua ya kuwa mimi ni YEHOVA, Mungu wenu, niwakomboaye mtoke chini ya mizigo ya Wamisri.


Bwana MUNGU asema hivi; Nitakapokuwa nimewakusanya nyumba ya Israeli, na kuwatoa katika watu ambao wametawanyika kati yao, na kutakasika kati yao machoni pa mataifa, ndipo watakapokaa katika nchi yao wenyewe, niliyompa mtumishi wangu, Yakobo.


Haya ndiyo aliyonionesha; na tazama, Bwana alisimama karibu na ukuta uliojengwa kwa timazi, mwenye timazi mkononi mwake.


Mimi ni Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo? Mungu si Mungu wa wafu, bali wa walio hai.


Wala hakumpa urithi humu hata kiasi cha kuweka mguu; akaahidi kwamba atampa, iwe milki yake, na ya uzao wake baadaye alipokuwa hana mtoto.


Angalieni, nimewawekea nchi mbele yenu, ingieni mkaimiliki nchi BWANA aliyowaapia baba zenu, Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, kwamba atawapa na uzao wao baada yao.


BWANA akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko.


Si kwa haki yako, wala kwa unyofu wa moyo wako, hivi uingiavyo kuimiliki nchi yao; lakini ni kwa uovu wa mataifa haya BWANA, Mungu wako, awafukuza nje mbele yako; tena apate kuliweka imara hilo neno BWANA alilowaapia baba zako Abrahamu, na Isaka, na Yakobo.


Lakini sasa wanaitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo