Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mwanzo 25:30 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

30 Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Kwa hiyo akamwambia Yakobo, “Nafa njaa; tafadhali, nigawie chakula hicho chekundu nile.” (Ndiyo maana walimpanga jina Edomu yaani mwekundu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Kwa hiyo akamwambia Yakobo, “Nafa njaa; tafadhali, nigawie chakula hicho chekundu nile.” (Ndiyo maana walimpanga jina Edomu yaani mwekundu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Kwa hiyo akamwambia Yakobo, “Nafa njaa; tafadhali, nigawie chakula hicho chekundu nile.” (Ndiyo maana walimpanga jina Edomu yaani mwekundu).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Esau akamwambia Yakobo, “Haraka, nipe huo mchuzi mwekundu! Nina njaa kali sana!” (Hii ndiyo sababu pia aliitwa Edomu.)

Tazama sura Nakili

Mwanzo 25:30
15 Marejeleo ya Msalaba  

Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka mbugani, naye alikuwa amechoka sana.

Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza.

Basi, Yakobo akapeleka wajumbe mbele yake kwenda kwa Esau nduguye mpaka nchi ya Seiri katika nyika ya Edomu.

Akawaagiza akisema, Mwambieni hivi bwana wangu, Esau, Hivi ndivyo asemavyo mtumwa wako, Yakobo; Nimekaa ugenini kwa Labani, na kukawia huko hata sasa,

Hivi ndivyo vizazi vya Esau, ndiye Edomu.

Hao ni wana wa Esau, na hao ndio majumbe wao; naye Esau ndiye Edomu.

jumbe Magdieli, jumbe Iramu. Hao ndio majumbe wa Edomu, kulingana na makao yao, katika nchi ya mamlaka yao. Naye huyo ndiye Esau, baba ya Edomu.

Esau akakaa katika mlima Seiri, Esau ndiye Edomu.

Hivi ni vizazi vya Esau, baba ya Edomu katika mlima Seiri.

Zamani zake, Edomu wakaasi mkononi mwa Yuda, wakajifanyia mfalme.

Ndipo majumbe wa Edomu wakashangaa, Watu wa Moabu wenye nguvu tetemeko limewapata, Watu wote wakaao Kanaani wameyeyuka.

Kuhusu Edomu. BWANA wa majeshi asema hivi, Je! Hakuna tena hekima katika Temani? Mashauri yamewapotea wenye busara? Je! Imetoweka hekima yao?

Maono yake Obadia. Ndivyo asemavyo Bwana MUNGU juu ya Edomu; Tumepata habari kwa BWANA, Na mjumbe ametumwa kati ya mataifa, Akisema, Haya, inukeni ninyi; Na tuinuke tupigane naye.

Usimchukie Mwedomi; kwa kuwa ni ndugu yako; usimchukie Mmisri, kwa kuwa ulikuwa mgeni katika nchi yake.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo