Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mwanzo 25:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

26 Baadaye ndugu yake akatoka, na mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino. Akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini mkewe alipowazaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Wa pili alizaliwa akiwa amemshika Esau kisigino, hivyo wakampa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati Esau na Yakobo walipozaliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Wa pili alizaliwa akiwa amemshika Esau kisigino, hivyo wakampa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati Esau na Yakobo walipozaliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Wa pili alizaliwa akiwa amemshika Esau kisigino, hivyo wakampa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini wakati Esau na Yakobo walipozaliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina Yakobo. Isaka alikuwa na umri wa miaka sitini Rebeka alipowazaa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Baadaye, ndugu yake akatoka, mkono wake ukiwa umemshika Esau kisigino; akaitwa jina lake Yakobo. Isaka alikuwa mwenye miaka sitini Rebeka alipowazaa.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 25:26
13 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Abrahamu alikuwa mtu wa miaka mia moja, alipozaliwa mwana wake Isaka.


Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.


Akasema, Je! Hakuitwa Yakobo kwa haki, maana amejitia mahali pangu mara mbili hizi? Alichukua haki yangu ya mzaliwa wa kwanza, na sasa ameichukua baraka yangu. Akasema, Je! Hukuniwekea na mimi mbaraka?


Siku za Isaka zilikuwa miaka mia moja na themanini.


Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.


Tumboni alimshika ndugu yake kisigino; Na alipokuwa mtu mzima alishindana na Mungu;


Naam, alishindana na malaika Akashinda; alilia, na kumsihi; Alimwona huko Betheli, naye akasema nasi huko;


Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo;


Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata;


Akampa agano la tohara; basi Abrahamu akamzaa Isaka, akamtahiri siku ya nane. Isaka akamzaa Yakobo. Yakobo akawazaa wale kumi na wawili, wazee wetu.


Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa BWANA.


Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo