Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mwanzo 25:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

25 Wa kwanza akatoka, naye alikuwa mwekundu mwili wote kama vazi la nywele. Wakamwita jina lake Esau.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Wa kwanza alikuwa mwekundu, mwenye nywele mwili wote; hivyo wakamwita Esau.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Wa kwanza alikuwa mwekundu, mwenye nywele mwili wote; hivyo wakamwita Esau.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Wa kwanza alikuwa mwekundu, mwenye nywele mwili wote; hivyo wakamwita Esau.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, na mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina Esau.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Wa kwanza kuzaliwa alikuwa mwekundu, mwili wake wote ulikuwa kama mtu aliyevaa vazi lenye nywele; wakamwita jina lake Esau.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 25:25
10 Marejeleo ya Msalaba  

Siku zake za kuzaa zilipotimia, tazama! Mapacha walikuwamo tumboni mwake.


Ikawa Isaka alipokuwa mzee, na macho yake yamepofuka asione, akamwita Esau, mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu. Naye akamwitikia, Mimi hapa.


Yakobo akamwambia Rebeka mamaye, Esau ndugu yangu ni mtu mwenye malaika, na mimi ni mtu laini.


Na ngozi za wana-mbuzi akamvika mikononi, na katika ulaini wa shingo yake.


Wala hakumtambua, kwa maana mikono yake ilikuwa kama mikono ya Esau, ndugu yake, yenye malaika; basi akambariki.


Na Abrahamu naye akamzaa Isaka. Wana wa Isaka; Esau, na Israeli.


Nimewapenda ninyi, asema BWANA. Lakini ninyi mwasema, Umetupendaje? Je! Esau siye ndugu yake Yakobo? Asema BWANA; ila nimempenda Yakobo;


Kisha Musa akatuma wajumbe kutoka Kadeshi wamwendee mfalme wa Edomu, na kusema, Ndugu yako Israeli asema, Wewe wazijua taabu zote zilizotupata;


Wana wao watakaozaliwa kizazi cha tatu na waingie katika mkutano wa BWANA.


Kisha nikampa huyo Isaka, Yakobo na Esau; nami nikampa Esau mlima Seiri aumiliki; Yakobo na watoto wake wakashuka Misri.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo