Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 25:21 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

21 Isaka akamwomba BWANA kwa ajili ya mke wake, maana alikuwa tasa. Naye BWANA akamwitikia, na Rebeka mkewe akachukua mimba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Rebeka alikuwa tasa, kwa hiyo Isaka akamwomba Mwenyezi-Mungu. Naye Mwenyezi-Mungu akakubali ombi lake, Rebeka akapata mimba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Rebeka alikuwa tasa, kwa hiyo Isaka akamwomba Mwenyezi-Mungu. Naye Mwenyezi-Mungu akakubali ombi lake, Rebeka akapata mimba.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Rebeka alikuwa tasa, kwa hiyo Isaka akamwomba Mwenyezi-Mungu. Naye Mwenyezi-Mungu akakubali ombi lake, Rebeka akapata mimba.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Isaka akamwomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. Mwenyezi Mungu akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Isaka akamwomba bwana kwa ajili ya mke wake, kwa sababu alikuwa tasa. bwana akajibu maombi yake na Rebeka mkewe akapata mimba.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 25:21
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.


Sarai akamwambia Abramu, kwa kuwa BWANA amenifunga tumbo nisizae, sasa mwingilie mjakazi wangu, labda nitapata uzao kutoka kwake. Abramu akaisikiliza sauti ya Sarai.


Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo.


Wakapata msaada juu yao, nao Wahajiri walitiwa mikononi mwao, na wote waliokuwa pamoja nao; kwa kuwa walimlingana Mungu pale vitani; naye akayatakabali maombi yao, kwa sababu walimtumaini yeye.


Akamwomba; naye akamtakabali, akayasikia maombi yake; akamrudisha tena Yerusalemu katika ufalme wake. Ndipo Manase akajua ya kwamba BWANA ndiye Mungu.


Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.


Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA, Uzao wa tumbo ni thawabu.


Hutimiza matakwa ya wote wamchao, Na pia husikia kilio chao, na huwaokoa.


Uniite siku ya mateso; Nitakuokoa, nawe utanitukuza.


Wewe usikiaye maombi, Wote wenye mwili watakujia.


Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni, Nitamwokoa na kumtukuza;


Aogopacho mtu asiye haki ndicho kitakachomjilia; Na wenye haki watapewa matakwa yao.


BWANA, Mtakatifu wa Israeli, na Muumba wake, asema hivi; Niulize habari za mambo yatakayokuja; mambo ya wana wangu, na habari ya kazi ya mikono yangu; haya! Niagizeni.


Ndipo utaita, na BWANA ataitika; utalia, naye atasema, Mimi hapa. Kama ukiiondoa nira; isiwepo kati yako, wala kunyosha kidole, wala kunena maovu;


Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa bado wanena, nitasikia.


Lakini yule malaika akamwambia, Usiogope, Zakaria, maana dua yako imesikiwa, na mkeo Elisabeti atakuzalia mtoto wa kiume, na jina lake utamwita Yohana.


Nao walikuwa hawana mtoto, maana Elisabeti alikuwa tasa, na wote wawili ni wazee sana.


Akaweka nadhiri, akasema, Ee BWANA wa majeshi, ikiwa wewe utayaangalia mateso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto wa kiume, ndipo mimi nitakapompa BWANA huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikia kichwani kamwe.


Ndipo Eli akajibu, akasema, Nenda kwa amani; na Mungu wa Israeli akujalie haja yako uliyomwomba.


naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto.


Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo