Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 24:49 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

49 Basi, kama mnataka kumfanyia rehema na kweli bwana wangu, niambieni kama sivyo, niambieni; ili nigeuke upande wa kulia au wa kushoto.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

49 Sasa, basi, niambieni kama mko tayari kumtendea bwana wangu kwa uaminifu na haki; kama sivyo, basi semeni, nami nitajua cha kufanya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

49 Sasa, basi, niambieni kama mko tayari kumtendea bwana wangu kwa uaminifu na haki; kama sivyo, basi semeni, nami nitajua cha kufanya.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

49 Sasa, basi, niambieni kama mko tayari kumtendea bwana wangu kwa uaminifu na haki; kama sivyo, basi semeni, nami nitajua cha kufanya.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

49 Ikiwa mtaonesha wema na uaminifu kwa bwana wangu, mniambie; la sivyo, mniambie, ili niweze kujua njia ya kugeukia.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

49 Ikiwa mtaonyesha wema na uaminifu kwa bwana wangu, mniambie, la sivyo, mniambie, ili niweze kujua njia ya kugeukia.”

Tazama sura Nakili




Mwanzo 24:49
6 Marejeleo ya Msalaba  

mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote na kweli yote uliyomfanyia mtumwa wako; maana nilivuka mto huo wa Yordani na fimbo yangu tu, na sasa nimekuwa makundi mawili.


Siku za kufa kwake Israeli zikakaribia; akamwita mwanawe Yusufu, akamwambia, Kama nimeona kibali machoni pako, weka mkono wako chini ya paja langu, ukanifanyie rehema na kweli; nakusihi usinizike katika Misri.


Rehema na kweli zisiachane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu ya kibao cha moyo wako.


tafadhali utupe ruhusa tupite katika nchi yako; hatutapita katika mashamba, wala katika mashamba ya mizabibu, wala hatutakunywa maji ya visimani; tutaifuata njia kuu ya mfalme, tusigeuke kwenda upande wa kulia, wala upande wa kushoto, hadi tutakapotoka katika nchi yako.


Nipishe katikati ya nchi yako; nitakwenda kwa njia ya barabara, sitageuka kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto.


Wale wanaume wakamwambia, Tutautoa uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa hisani na uaminifu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo