Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Mwanzo 24:48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

48 Nikainama, nikamsujudia BWANA, nikamtukuza BWANA, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, aliyeniongoza njiani, nimtwalie mwana wa bwana wangu binti wa ndugu yake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

48 Kisha nikainama na kumwabudu Mwenyezi-Mungu; nikamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye ameniongoza moja kwa moja kwa binti wa ukoo wa bwana wangu kwa ajili ya mwanawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

48 Kisha nikainama na kumwabudu Mwenyezi-Mungu; nikamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye ameniongoza moja kwa moja kwa binti wa ukoo wa bwana wangu kwa ajili ya mwanawe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

48 Kisha nikainama na kumwabudu Mwenyezi-Mungu; nikamtukuza Mwenyezi-Mungu, Mungu wa bwana wangu Abrahamu, ambaye ameniongoza moja kwa moja kwa binti wa ukoo wa bwana wangu kwa ajili ya mwanawe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

48 nikasujudu na nikamwabudu Mwenyezi Mungu. Nikamtukuza Mwenyezi Mungu, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

48 nikasujudu na nikamwabudu bwana. Nikamtukuza bwana, Mungu wa bwana wangu Ibrahimu, aliyeniongoza katika njia sahihi ili nimtwalie mwana na bwana wangu mke katika jamaa zake.

Tazama sura Nakili

Mwanzo 24:48
11 Marejeleo ya Msalaba  

Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu.

Ikawa mtumishi wa Abrahamu aliposikia maneno yao, akainama hata nchi mbele za BWANA.

Ndipo nikaamuru kufunga, hapo penye mto Ahava, ili tupate kujinyenyekeza mbele za Mungu, na kutafuta kwake njia iliyonyoka, kwa ajili yetu sisi wenyewe, na kwa ajili ya watoto wetu, na kwa mali yetu yote.

Akawaongoza kwa njia ya kunyoka, Wapate kwenda mpaka mji wa kukaa.

Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; Nitakushauri, jicho langu likikutazama.

Kwa maana ndivyo alivyo MUNGU, Mungu wetu. Milele na milele Yeye ndiye atakayetuongoza.

nawe utawafundisha zile amri na sheria, nawe utawaonesha njia ambayo inawapasa kuiendea, na kazi ambayo inawapasa kuifanya.

Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu.

BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo