Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Mwanzo 24:29 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

29 Na Rebeka alikuwa na kaka, jina lake Labani. Labani akatoka mbio kumwendea yule mtu kisimani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 Rebeka alikuwa na kaka yake aitwaye Labani. Labani akatoka mbio kukutana na yule mtu kisimani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 Rebeka alikuwa na kaka yake aitwaye Labani. Labani akatoka mbio kukutana na yule mtu kisimani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 Rebeka alikuwa na kaka yake aitwaye Labani. Labani akatoka mbio kukutana na yule mtu kisimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani; huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 Rebeka alikuwa na kaka aliyeitwa Labani, huyo akaharakisha kukutana na yule mtumishi kule kisimani.

Tazama sura Nakili




Mwanzo 24:29
8 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa, alipoiona ile pete, na vikuku mikononi mwa dada yake, akasikia maneno ya Rebeka dada yake, akisema, Hivyo ndivyo alivyoniambia mtu huyo, basi akamjia mtu yule, na tazama, amesimama karibu na ngamia kisimani.


Kaka yake na mama yake wakasema, Msichana na akae kwetu kama siku kumi, zisipungue, baadaye aende.


Wakambariki Rebeka, wakamwambia, Dada yetu, wewe uwe mama wa elfu kumi, mara elfu nyingi, na wazao wako waurithi mlango wa hao wawachukiao.


Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.


Na sasa, mwanangu, sikia sauti yangu, uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani;


Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.


Ikawa Labani aliposikia habari za Yakobo, mwana wa nduguye, akaenda mbio amlaki, akamkumbatia, akambusu, akamleta nyumbani kwake. Naye akamwambia Labani maneno hayo yote.


Akawauliza, Je! Mnamjua Labani, mwana wa Nahori? Wakasema, Tunamjua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo